Raia wa Côte d’Ivoire leo Jumamosi Oktoba 25 wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura kote nchini kumchagua rais wao mpya. Wagombea watano wako kwenye kinyang’anyiro, akiwemo Rais aliyepo madarakani, Alassane Ouattara, ambaye anagombea muhula wa nne.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Pointi Muhimu

► Karibu wapiga kura milioni 8.7 wanatarajiwa kupiga kura leo Jumamosi hii, Oktoba 25, kumchagua rais mpya wa Côte d’Ivoire.

► Wagombea watano wanawania wadhifa wa rais: Alassane Ouattara, Rais aliyepo madarakani; Jean-Louis Billon, mpinzani kutoka chama cha PDCI; Simone Ehivet, mke wa zamani wa Laurent Gbagbo, kutoka chama cha Movement of Capable Generations; Ahoua Don Mello mwenye msimamo mkali; na Henriette Lagou mwenye msimamo wa kati.

► Viongozi wawili wakuu wa upinzani, Laurent Gbagbo na Tidjiane Thiam, hawashiriki uchaguz huo. Ugombea wao ulibatilishwa. Kutengwa kwao kwenye uchaguzi kumesababisha mvutano nchini. Maandamano yaliyoitishwa na Common Front—jukwaa linalounganisha Chama cha Kidemokrasia cha Côte d’Ivoire (PDCI) na Chama cha PPA-CI—yalipigwa marufuku na mamlaka na kukandamizwa. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani yaCôte d’Ivoire, zaidi ya watu 700 walikamatwa na zaidi ya waandamanaji 30 walihukumiwa kifungo jela.

Maafisa wa polisi na wanajeshi 44,000 wametumwa kulinda vituo 25,000 vya kupigia kura na kuzuia ghasia kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *