
Vyama vya wapinzani hao vimethibitisha kukamatwa kwao, wakiwa miongoni mwa wanachama wakuu wa Muungano wa jukwaa la mabadiliko ya kisiasa uliomuidhinisha mgombea Issa Tchiroma Bakary pamoja na madai yake ya kumshinda Rais Paul Biya wakati wa uchaguzi wa Oktoba 12.
Chama cha Vuguvugu la Afrika la Uhuru na Demokrasia Mpya (MANIDEM) pia kimesema mlinda hazina wake na wanachama wengine walitekwa nyara na vikosi vya usalama vya ndani. Kimesema lengo la hatua hiyo ni kuwatishia raia wa nchi hiyo.
Hata hivyo mazingira ya kukamatwa kwao hayakuwekwa wazi mara moja.
Katika siku za hivi karibuni, upinzani umefanya maandamano na kuonya dhidi ya jaribio la wizi wa kura.