
Ukraine imelengwa tena na mashambulizi ya Urusi katika saa za hivi karibuni. Vitongoji kadhaa huko Kyiv vimelengwa na mashambulizi haya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mara nyingine tena, mamilioni ya wakazi wa mji mkuu wamelazimika kulala katika majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya awali ya Urusi. Mtu mmoja ameuawa na wengine saba wamejeruhiwa. Katika Jimbo la Dnipropetrovsk, mkuu wa utawala wa kijeshi katika jimbo hilo amesema watu wawili wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa katika mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani.
Milipuko imesikika huko Kyiv mapema saa 10 alfajiri. Moto ulizuka katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu. Mashambulizi haya mapya ya Urusi yanakuja huku nchi hiyo ikiwa tayari imeingia gizani na baridi kufuatia mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya nishati katika wiki za hivi karibuni. Na mashambulizi hayo yanaongezeka kwa nguvu na mara kwa mara, anaripoti mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze.
Siku ya Ijumaa, Jimbo la Odessa lilikumbwa kwa mara ya kwanza na mabomu ya angani yaliyoongozwa, mabomu yaliyobeba kilo 250, wakati mwingine kilo 500 za vilipuzi, yaliyotumiwa na Urusi kuharibu ngome za wanajeshi wa Ukraine kwenye mstari wa mbele na kuteketeza miji iliyopo. Jiji la Kherson pia lililengwa na mabomu mabomu, na kuwaua watu wanne. Tangu kukombolewa kwake na Kyiv mnamo mwezi Novemba 2022, baada ya miezi sita ya mashambulizi ya Urusi, jiji hilo, lililoko kwenye kingo za Mto Dnieper, ambao ni mstari wa mbele katika eneo hili, limekuwa likishambuliwa karibu kila siku na vikosi vya Urusi. Na katika eneo hilo la Kherson, sintofahamu inaendelea upande wa Urusi.
Raia wanalengwa na ndege zisizo na rubani
Wiki hii, kulikuwa na hisia nyingi nchini Ukraine wakati picha za Larysa Vakuliuk, mfugaji wa mbuzi mwenye umri wa miaka 84 aliyeuawa barabarani katika mashamba lake, pamoja na mbuzi wake wawili. Aliuawa na moja ya ndege hizi zisizo na rubani. Alikuwa amekataa kuondoka katika jamii yake licha ya hatari ili kuepuka kuwaacha wanyama wake. Hii ni moja ya kesi miongoni mwa mamia ya nyingine zinazoonyesha Urusi ikilenga raia wa Ukraine, kinyume na sheria za kimataifa.