London, England. Arsenal imeendelea kuonyesha nia ya kuhitaji Ubingwa wa EPL msimu huu baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace kwenye Uwanja wa Emirates, London.

Bao pekee la washika mitutu hao limefungwa na Eberechi Eze katika dakika ya 39 ambaye alizamisha mpira wavuni na kuifunga Crystal Palace ambayo alikuwa akiitumikia msimu uliopita kabla ya kujiunga na The Gunners.

Baada ya kuondoka na ushindi huo vijana wa Mikel Arteta sasa wameongeza tofauti ya pointi kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakifiskisha pointi 22 ikiwa ni tofauti ya pointi nne dhidi ya Bournemouth ambayo inashika nafasi ya pili kwa pointi 18.

Arsenal itakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani tena Oktoba 29, 2025 kuvaana na Brighton kwenye Kombe la Karabao kabla ya kuiharika Burnley Novemba Mosi katika mechi ya EPL kisha kusafiri kwenda Jamuhuri ya watu wa Czech kuivaa Slavia Plague katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayofanyika Novemba 4, 2025.

Man City yachezea kipigo

Katika mechi nyingine iliyochezwa leo imeshuhudiwa timu ya Pep Guardiola, Man City ikikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Villa Park, Billingham dhidi ya Aston Villa.

Bao pekee la Aston Villa limefungwa na Matty Cash katika dakika ya 19 akimalizia kwa uzuri pasi ya kiungo Muargentina, Emiliano Buendia.

Villa imesogea hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa EPL ikifikisha pointi 15 wakati Man City ikitelemka hadi nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 sawa na mahasimu wao Man United ambao wapo nafasi ya tano.

Katika mechi nyingine zilizochezwa kwenye ligi hiyo pendwa zaidi duniani imeshuhudiwa Bounermouth ikiichapa Nottngham Forest mabao 2-0 wakati Wolverhampton ikiwa kwenye Uwanja wa nyumbani ikiondoka kwa aibu baada ya kushushiwa kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Burnley.

Mchezo mwingine utapigwa baadae saa 1:30 kwenye Uwanja wa Hill Dickinson, Liverpool ambapo Everton itawakaribisha, Tottenham.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *