#HABARI: Mgombea ubunge Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Profesa Adolf Mkenda amewahimiza wananchi wa Vijiji vya Wilaya ya Rombo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kupiga kura na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya katika Wilaya hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara,ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa, ujenzi wa shule ya amali mabweni ya kisasa.

Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakazi wa wilaya ya Rombo wameonesha mwamko na imani kubwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wakinadi sera katika vijiji vya wilaya hiyo na hivyo wanaimani Dkt. Samia Suluhu Hassan atashinda kwa kishindo katika jimbo hilo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *