A Hamas member holding a gun

Je, Hamas inaweza kujiimarisha upya baada ya masaibu ya Israel?

    • Author, Paul Adams
    • Nafasi, Diplomatic correspondent
    • Author, Rushdi Abualouf
    • Nafasi, Gaza correspondent

Je, ni kwa namna gani kundi ambalo limetawala Ukanda wa Gaza kwa takriban miaka 20, likiowangoza Wapalestina milioni mbili kwa mkono wa chuma na kupigana na Israel mara kwa mara, ghafla linaweka chini silaha zake na kuachia madaraka?

Kwa kuzingatia mtiririko wa picha za kutisha zinazoibuka kutoka Gaza tangu usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa tarehe 10 Oktoba, Hamas inaonekana kuwa na nia ya kurejesha mamlaka yake.

Wapiganaji wake waliofunika nyuso wamerejea mitaani, wamekuwa wakionekana wakiwapiga na kuwaua wapinzani.

Waathiriwa wengine, wale wanaoonyesha uoga, wanapigwa risasi za miguuni kupigwa kwa marungu.

Baadhi ya wale ambao wanashambuliwa na Hamas ni wale walikuwa sehemu ya makundi yaliyohusika na wizi wa misaada, kulingana na mfanyakazi mmoja wa mashirika ya kutoa misaada ambaye alizungumza na BBC. Umoja wa Mataifa pia imeyashutumu magenge ya wahalifu yanayoiba vyakula vya misaada.

Mazingira yaliyopo kwa sasa hayawezi kutatoa fursa kwa wapiganaji wa Hamas kuweka silaha chini na kukabidi mamlaka ya Gaza kwa kikosi cha kimataifa cha kudumisha amani kama ilivyopendekeza katika mpango wa amani wa Trump wenye vipengele 20.

 Mwanamgambo wa Hamas akipeperusha bendera ya chama chake

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Rais Trump hapo awali alionekana kutoelewana suala hilo.

Alipokuwa nnjiani kuelekea Israel mnamo Oktoba 13, aliashiria kuwa Marekani imeipatia Hamas -iliyoorodheshwa kuwa kundi la kigaidi na Marekani Uingereza, Israel na mataifa mengine – idhini ya kurejesha hali ya utulivu.

“Tumewapa idhini kwa muda,” aliwaambia waandishi wa habari wakati alipokuwa aki ndege ya Air Force One.

Siku tatu baadaye, akabadili msimamo. “Ikiwa Hamas itaendelea kuwaua watu Gaza, hatua ambayo haikuwa sehemu ya makubaliano,” aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, “hatutakuwa na budi ila kuingia nakuwaangamiza.”

Je, hali ya sasa huko Gaza inawaacha wapi Hamas?

Na hatimaye, baada ya miaka miwili ya vita ambayo imesababisha mateso yasiyo na kifani kwa watu wake wenyewe na vifo vingi vya wakuu wake wa ngazi ya juu, ni nini hatma ya kundi hilo?

‘Kusambaratika kabisa kwa utawala wa sheria’

Wakaazi wengi wa Gaza, wameumizwa na kuchoshwa na miaka miwili ya mateso yasio na kikomo – ya vita ambavyo vimesababisha vifo vya takriban watu 68,000 huko Gaza kulingana na Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas – mwisho huu mbaya unatia wasiwasi, lakini haishangazi.

Kati ya Wagaza ambao mwandishi wetu alizungumza nao – miongoni mwao, wafanyakazi wa misaada, wanasheria, pamoja na mshauri wa zamani wa kiongozi wa Hamas – kila mmoja ana mtazamo tofauti juu ya uwezekano wa Hamas kuweka silaha chini na kuachia udhibiti.

Bila shaka – kwa kuzingatia hali ilivyo – Sasa ni hawana budi kufanya hivyo.


Wapalestina walikusanyika kusherehekea kufuatia kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

Imekuwa miaka miwili ya ukosefu wa utawala wa sheria na utulivu,” mfanyakazi wa misaada Hanya Aljamal anasema kutoka nyumbani kwake Deir al-Balah, katikati ya Ukanda wa Gaza. “Tunahitaji mtu mwingine kusimamia uogozi.

“Japo Hamas hawana sifa za kutawala Ukanda huo, heri wao kuliko kuongozwa na magenge.”

Dk Ahmad Yousef, mshauri wa zamani wa Ismail Haniyeh, ambaye alikuwa kiongozi wa kisiasa wa Hamas, ana maoni kwamba mshiko thabiti unahitajika kwa sasa.

“Maadamu bado kuna watu wanaojaribu kuchukua sheria mikononi mwao, tunahitaji mtu wa kuwatishia na kuwawajibisha,” anasema Dk Yousef, ambaye sasa anaendesha chombo cha ushauri cha Gaza na kuwa karibu na uongozi wa Hamas.

A shot of Hanya Aljamal

“Hii itachukuwa muda. Sio muda mrefu.Ndani ya mwezi mmoja tutaleta vikosi vya polisi na kijeshi kutoka Uturuki na Misri,” anaendelea kusema akiashiria kikosi cha kimataifa ya kufuatilia hali ya usalama Gaza, kama ilivyoratibiwa katika mpango wa amani, ambacho kitajumuisha wanajeshi kutoka Misri na Uturuki miongoni mwa mataifa mengine.

“Huo ndio wakati wataweka kando silaha zao.”

Baadhi ya wakaaziwa Gaza wanatilia shaka mpango huo na wanaishi kwa uwoga. Wengine wao wanaamini kuwa Hamas haitakubali kuachia madarka – au kuweka chini silaha

Moumen al-Natour, wakili wa Gaza aliyefungwa mara kadhaa na Hamas, ni mmoja wao.


Wanachama wa Hamas wakipanga foleni

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Amekuwa mafichoni tangu Julai, anaposema kuwa wapiganaji wa kundi la Hamas waliojifunika nyuso zao walikuja kwenye nyumba yake jijini Gaza na kumwamuru kuripoti katika hospitali ya al-Shifa kwa mahojiano.

“Hamas [inatuma] ujumbe kwa ulimwengu na kwa Rais Donald Trump … kwamba hawataachia mamlaka au kusalimisha silaha zao.

“Ningeangukia mikononi mwa Hamas muda huu, watatengeneza video na kuniua barabarani kwa kunipiga risasi ya kichwa,” anasema katika moja wapo wa video kadhaa tulizotumiwa kutoka eneo lisilojulikana katika Ukanda wa Gaza.

Ukuta uliyo nyuma yake umejaa matundu ya risasi.

Moumen al-Natour

“Ni genge la wahalifu, sio serikali,” anasema akiashiria kundi la Hamas.

“Sitaki wasalie Gaza… Siwataki serikalini, na sitaki wawe sehemu walinda usalama. Sitaki kuona itikadi zao zikienezwa misikitini, mitaani au shuleni.”

‘Bado ni mshirika mkuu Gaza’

Bw al-Natour ana mtazamo wake mwenyewe kuhusu jinsi Gaza itakavyoweza kusonga mbele.

Vikosi tofauti vya wanamgambo vinavyohudumu chini ya Hamas vinaweza, kwa mtazamo wake, kuunganishwa kuwa chombo kipya cha usalama. Lakini pamoja na ajenda zao zinazokinzana, mazingira magumu waliyopitia, katika baadhi ya matukio, uhusiano wenye utata kwa jeshi la Israel, hilo litakuwa pendekezo gumu.

“Ukweli ni kwamba – na wakati mwingine ni vigumu sana kwa Waisrael kukiri hili – kwamba Hamas bado ipo na ndiyo mhusika mkuu huko Gaza.” Anasema Dk Michael Milshtein, mkuu wa zamani wa idara ya Masuala ya Palestina katika Ujasusi wa Kijeshi wa Israel.

“Kutegemea wahusika wanaotiliwa shaka – koo, wanamgambo, magenge, baadhi yao wahalifu, wengine wao wakiwa na uhusiano na ISIS [kundi la Islamic State], wengi wao wakihusika katika mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Israel – na kuwachukulia kama aina mbadala ya Hamas ni udanganyifu.”

Dk Michael Milshtein akitabasamu

Maafisa wa Hamas wamesema kundi hilo liko tayari kuachia udhibiti wa kisiasa wa Gaza. Mpango wa kusitisha mapigano wa Trump, ambao ulitoa uungaji mkono wake, unalenga “utawala wa mpito wa muda wa kamati maalum ya Palestina isiyoegemea upande wowowte wa kisiasa”.

Lakini hata kama kundi hilo liko tayari kurejea nyuma katika jukumu lake la kisiasa – jambo ambalo Wapalestina na Waisraeli wengi bado wanatilia shaka – kuwashawishi wapiganaji wake walio na na uwezo wa kupigana vita kali kuweka chini silaha zao ni hatua kubwa kwa kundi ambalo nguvu yake, hata kabla ya Oktoba 2023, ilitegemea sana silaha.

Chimbuko la Hamas na uongozi wake thabiti

Kuanza kujibu swali tata la ni ipi hatma ya Hamas kunahitaji kurudi nyuma katika jinsi gani hasa iliimarisha mamlaka hapo kwanza.

Kutoka asili yake katika miaka ya 1980 kama kitengo kilichojitenga na cha kundi la Muslim Brotherhood wa Misri na mpinzani wa Chama chacha Ukombozi wa Palestina (PLO), Hamas ilibadilika na kuwa kundi la wanamgambo waliohusika na vifo vya raia wa Israel.

Hapo awali, Israel iliungwaji mkono Hamas kisiri, ikiiona kama kiungo muhimu cha kukabiliana na PLO na kundi lake kuu la Fatah, lililoongozwa wakati huo na Yasser Arafat.

“Adui mkubwa alikuwa Fatah,” anasema Ami Ayalon, mkuu wa zamani wa huduma ya usalama ya ndani ya Israeli, Shin Bet, “kwa sababu walikuwa watu ambao walipigania uhuru wa taifa la Palestina.”

Lakini Hamas ilipoanzisha mashambulizi mabaya ya mabomu ya kujitoa mhanga katika miaka ya 1990 na 2000 dhidi ya Waisraeli, Israel ilijibu kwa mfululizo wa mauaji ya hali ya juu.

Mgogoro mkali wa madaraka na Fatah uliiacha Hamas, ambayo ilishinda uchaguzi wa 2006, kama mdhibiti pekee wa Ukanda wa Gaza.

A map showing where Gaza is, as well as Egypt and Israel

Miaka kumi na minane ya utawala wa Hamas iulikumbwa na sifa ya vikwazo vya kijeshi na kiuchumi vya Israel, na mizozo ya kivita mwaka 2008-09, 2012, 2014 na 2021.

Licha ya madai ya Israel tangu Oktoba 2023 kuwa “Hamas ni ISIS”, serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hapo awali ilijiridhisha kuwa Hamas haikuwa tishio la kimkakati.

“Yake ilikuwa sera ya kudhibiti mzozo,” anasema Bw Ayalon. “Alisema hatutasuluhisha na tunapingana kuzuia uwepo wa serikali mbili, kwa hivyo njia pekee ni kuvuruga na kudhibiti.

Huku Hamas ikitawala Gaza na Mamlaka ya Palestina, inayoongozwa na Rais Mahmoud Abbas, ikitawala katika sehemu ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Wapalestina walijipata katikati ya mgawanyiko usio na matumaini, na hivyo kuiwezesha Israel kutoa hoja kwamba haina uongozi wa pamoja wa kufanya nao mazungumzo ya amani.

“[Netanyahu] alifanya kila awezalo ili kuunga mkono Hamas huko Gaza,” Bw Ayalon anasema. “Aliiruhusu Qatar iwatume… zaidi ya $1.5bn.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Chanzo cha picha, Getty Images

Pesa hizo kutoka Qatar zilikusudiwa kulipa mishahara ya watumishi wa umma na kusaidia familia maskini zaidi, lakini wakuu wa usalama walihofia kuwa zilikuwa zinatumika kwa malengo mengine.

Bw Ayalon anaongeza: “Ilikuwa wazi kwa mkurugenzi wa Shin Bet na mkuu wa Mossad kwamba pesa hizi zingeenda kwa miundombinu ya kijeshi.

Netanyahu ametetea kuruhusu malipo kwa Hamas, akisema ilikusudiwa kuwasaidia raia.

Hamas walikuwa wakijiandaa kwa vita

Mashambulizi ya tarehe 7 Oktoba yalifichua kwamba, Hamas imekuwa ikijiandaa kwa vita. Hili lilidhihirishwa na mtando wa mahandaki iliyokuwa imeweka tayari kwa chaochote kitakachotokea.

Mahandaki hayo yalikuwa yametumika kufanya mashambulizi dhidi ya jeshi la Israel wakati wa maasi ya pili ya Wapalestina, au “Intifada” yaliyoanza mwaka 2000.

Mnamo 2006, wapiganaji wa Hamas walitumia handaki chini ya mpaka na Israeli kushambulia kituo cha kijeshi karibu na Kerem Shalom, na kuua wanajeshi wawili wa Israeli na kumteka nyara wa tatu, Gilad Shalit.

Alishikiliwa kwa miaka mitano hadi kuachiliwa kwake, mnamo 2011, badala ya wafungwa 1,027 wa Kipalestina, akiwemo Yahya Sinwar, ambaye angeendeleza mashambulio ya Hamas ya Oktoba 2023.

Yahya Sinwar

Chanzo cha picha, Getty Images

Kadiri muda ulivyosonga, mtandao wa mahandaki ya Hamas ulipanuka, na kujumuisha karakana, maeneo ya kutengeneza silaha na vituo vya kutoa amri.

Maendeleo ya kikanda pia yalichangia. Mnamo mwaka wa 2012, baada ya kuanguka kwa dikteta wa Libya Muammar Gaddafi na kupanda kwa muda mfupi madarakani kwa Ikhwanul Muslimin nchini Misri, Hamas iliweza kusafirisha silaha za kisasa zaidi hadi Gaza, ikiwa ni pamoja na bunduki za sniper, kurusha roketi na vifaa vya kutengeneza roketi za masafa marefu.

Hamas inadhaniwa kunufaika kutokana na usaidizi wa mafundi na wapiganaji wenye uzoefu wa kufika hadi maeneo kama Lebanon na Iraq kupitia njia za chini kwa chini. Iran pia ilikuwa mshirika mkuu, ikiiona Hamasa kama kama sehemu ya asili yake katika ”Mhimili wa Upinzani,” na muungano wa makundi ya wapiganaji Mashariki ya kati yenye chuki ya pamoja dhidi ya Israel na Markani.

Mnamo mwaka 2020,ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa Iran ilitumia takriban dola milioni 100 za kimarekani kwa mwaka kufadhili makundi ya wanamgambo wa Kipalestina ikiwa ni pamoja na Hamas.

Mpiganaji akisemama mbele ya lango la handaki wakati wa maonyesho ya silaha

Chanzo cha picha, Yousef Masoud/SOPA Images/LightRocket via Getty Images

Baadhi ya mahandaki yaliripotiwa kuchimbwa kwa kina cha futi 230 (70m) chini ya ardhi, ilichukua miaka kadhaa kujengwa na kugharimu mamilioni ya dola kila moja. Mahandaki hayo yalijengwa kuwalinda makamanda wakuu wa Hamas na kuhifadhi silaha za masafa marefu.

Mtaalamu wa eneo hilo aliye na ufahamu wa kina wa mahandaki hayo aliiambia BBC kwamba gharama ya mradi mzima ilifikia takriban dola bilioni sita (£4.5bn).

Ni vigumu kupata takwimu sahihi, lakini inakadiriwa kuna mtandao wa mahandaki yaliyotawanyika umbali wa maili 250 (400km), katika ukanda wa ardhi wenye urefu wa maili 26 tu na, kwa upana wake zaidi, maili saba kwa upana.

Mahandaki: Mradi uliozingirwa na usiri

Ni hatia kujadili hadharani – eneo au gharama iliyotumika kwa ujenzi wa mahandaki hayo. Wakazi wa Gaza wanaofanya hivyo wanakabiliwa na hatari ya kutuhumiwa kwa ujasusi, kukamatwa na kuadhibiwa vikali. Lakini wengi walijua kinachoendelea.

Wakazi wa eneo hilo wangeona ishara: mchanga na udongo ukiondolewa, viingilio vipya vinavyojitokea mahali ambapo hapakutarajiwa na mashine zikiletwa nyakati za usiku giza.

Kilichoanza kama jibu la kutengwa kwa Gaza kikawa kipindi tata cha ujenzi wa viwanda na kambi za kijeshi za chini ya ardhi kwa miongo mitatu.

Ilibainika baadaye kwamba sehemu kubwa ilikuwa imefichwa chini ya miundombinu ya kiraia huko Gaza, ikiwa ni pamoja na hospitali, shule na katika visavingine ni ujenzi wa handaki lenye kituo cha data cha Hamas, makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi (UNRWA) katika Jiji la Gaza.

Palestinian flags are seen among the rubble of destroyed buildings

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

Baada ya tarehe 7 Oktoba 2023, wakati wapiganaji wa Hamas walipoivamia Israel, na kuwaua takriban watu 1,200 na kuchukua mateka wengine 251, pia iligeuka kuwa gereza kubwa la chini ya ardhi. Sio wote walioshikiliwa mateka walifichwa kwenye mahandaki hayo, lakini baadhi yao walishikiliwa humo, hasa wakati vita vilipokuwa vikiendelea.

Eli Sharabi, ambaye alikua mmoja wa watu mashuhuri zaidi waliotekwa kwanza alitolewa kutoka kwa nyumba salama na kupelekwa kwenye handaki baada ya siku 52 kati ya 491 alizokua kifungoni.

“Walitufunga kwa kamba miguuni na mikononi,” aliiambia BBC mapema mwezi huu. “Nilizimia mara kwa mara kutokana na maumivu. Kuna wakati walinivunja mbavu.”

Kufikia wakati alipoachiliwa huru, mnamo Februari, alikuwa amepungua zaidi ya kilo 30 (4st 10lb).

Wapiganaji wawili wa Hamas wakimsindikiza mateka wa Israel Eli Sharabi

Chanzo cha picha, EPA

Hamas waliwatumia mateka hao kama chambo cha, kushinikiza usitishaji wa mapigano au kuachiliwa kwa Wapalestina wanaozuiliwa katika magereza ya Israel.

Wakati mazungumzo juu ya hatma yao yakiendelea, Hamas iliwaumiza kisaikolojia jamaa za mateka wa Israel kwa kuvujisha mfululizo wa video za kikatili, mara nyingi zikiwaonyesha mateka katika hali ya dhiki.

Hatimaye ilikuwa, anasema Dk Yousef, shinikizo la ndani na nje ndilo lililowalazimu Hamas kuacha mkakati huo.

“Qatar, Misri na Uturuki na pia watu wa hapa katika kambi za wakimbizi walituma ujumbe mzito kwa viongozi wa Hamas kuwaambia jamani inatosha.”

Kiongozi wa zamani wa Hamas Ismail Haniyeh

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo, Israel ilikuwa inaendelea kuharibu kile inachoweza kwenye mtandao wa handaki, mara nyingi ikibomoa vitongoji vya kiraia katika mchakato huo.

Na kazi iko mbali sana.

“Kulingana na machapisho kutoka kwa taasisi ya ulinzi, makadirio yanazungumzia uharibifu wa kati ya 25% na 40% ya mahandaki,” anasema Yehuda Kfir, mhandisi wa kiraia wa Israel na mtafiti wa vita vya chinichini katika Chuo Kikuu cha Technion cha Haifa.

“Bila shaka [Hamas] inatamani kukarabati miundombinu, ikiwa ni pamoja na kurejesha mifereji ambayo iliharibiwa kwa njia mbalimbali na jeshi la Israel IDF.”

Uongozi kusambaratika

Kukarabati handaki ni kitu kimoja. Kufufua tena usimamizi wa ni kitu kingingine. Baada ya matukio ya miaka miwili iliyopita, uongozi wa Hamas imeachwa hoi.

Israel imechukua hatua kubwa zaidi – mjini Gaza, Iran, Lebanon na Qatar – kuwaangamiza wahusika wakuu wa kisiasa na kijeshi wa kundi hilo.

Kuanzia kwa viongozi wake maarufu zaidi, wanaotambulika kimataifa, wanaosafiri kote ulimwenguni kukuza malengo yao, hadi makamanda wa kikosi chake huko Gaza, Hamas imepoteza karibu kila mhusika muhimu.

Israel ilimuua kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa Hamas, Ismail Haniyeh, mjini Tehran mnamo Julai 2024.

Miezi mitatu baadaye, mrithi wa Haniyeh, Yahya Sinwar ambaye ni nadta kuonekana hadharani, aliuawa katika magofu ya nyumba huko Rafah.

Ismail Haniyeh, Yahya Sinwar na Saleh al-Arouri (kushoto kwenda kulia)

Chanzo cha picha, Reuters

Licha ya kuwapoteza viongozi hawa wakuu – na maelfu ya wanachama wa mrengo wake wa kijeshi- kundi kiliwasajili wapiganaji wa kizazi kipya wenye itikadi kali na kugawanyika katika makundi madogo kwa nia ya kutekeleza operesheni za kkuvizia.

Lakini tangu Oktoba 2025 Hamas imepata hasara kubwa baada ya shambulizi lake la Oktoba 7 dhidi ya Israel. Viongozi wa leo hawajulikani hivyo, muhimu zaidi, hawana uzoefu wa kisiasa.

Ezzedine al-Haddad, ambaye ana umri wa miaka 55, sasa anaongoza baraza la kijeshi lenye wanachama watano ambalo linaongoza tawi la Hamas lenye silaha, la vikosi vya Izz al-Din al-Qassam.

Michoro inayowaonyesha viongozi wa Hamas waliouawa (L-R) Ismail Haniyeh, Yahya Sinwar, Mohammed Deif na Sheikh Ahmed Yassin

Chanzo cha picha, EPA/ Shutterstock

Nje ya Gaza, uongozi wa kisiasa wa kundi hilo uliobaki ni pamoja na Khaled Meshaal (aliyekabiliwa na jaribio la mauaji la Israel huko Jordan mwaka 1997), Khalil al-Hayya na Muhammad Darwish.

Wote wanadaiwa kunusurika kifo tarehe 9 Septemba, wakati ndege za Israel ziliposhambulia jengo moja huko Doha, Qatar, ambapo walikuwa wakikutana kujadili mapendekezo ya hivi punde ya kusitisha mapigano ya Marekani.

Hamas ‘imechoshwa na vita’

Licha ya ghasia ambazo bado zinaendelea huko Gaza, mshauri wa zamani wa Hamas, Ahmed Yousef, anasema kundi hilo limechoshwa na vita.

Bila kutaja 7 Oktoba moja kwa moja, anaelezea sababu ya vita kama “kosa mbaya” na kwamba “mbinu tofauti” inahitajika.

Wanaume wawili wanaonekana hapa wakiwa wameketi mbele ya vifusi vya jengo liliporomoka huko Gaza

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

“Ninazungumza nao na baadhi yao na wamesema kuwa hawana nia ya kutawala tena Gaza,” anasema.

“Lakini Hamas ina wanachama zaidi ya wafuasi 100,000 na watu hao bila shaka hawatatoweka kirahisi kama inavyodhaniwa.”

Hamas, anapendekeza, inatazamia kujibadilisha ili kuendelea na jukumu la kisiasa katika siku zijazo, mchakato anaoufananisha na mabadiliko ya ANC kutoka vita vya msituni hadi utawala wa kisiasa Afrika Kusini baada ya enzi ya ubaguzi wa rangi.

“Endapo uchaguzi [ungelifanyika] kesho,” anasema , “Nina hakika Hamas itatumia jina lingine, kuonyesha kwamba wanazingatia amani zaidi na wako tayari kuwa sehemu uongozi wa kisiasa giving the impression it is more peaceful and more willing to be part of political life.

“Vurugu hazitakuwa sehemu ya chama chochote cha kisiasa.”

Dk Milshtein anasema.

“Hata kama kutakuwa na utawala mpya wa ndani huko Gaza, bila shaka nyuma ya pazia Hamas itakuwa mhusika mkuu,” anasema.

A press member looks at the Palestinian flag

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

Mpango wa kushinikiza kundi hilo kuweka chini silaha huenda usifanikiwe: anatabiri vita vingine vya Gaza ndani ya miaka mitano ijayo.

Lakini Ami Ayalon, mkuu wa zamani wa Shin Bet, anaamini Israel inapaswa kutafuta njia nyingine ya kukabiliana na adui yake.

“Tusiposhinda itikadi, zitastawi,” anasema.

“Njia pekee ya kukabiliana na itikadi kali ni kuwa na mpango utakao wahakikishia Wapalestina na watu wa Israel mustakabali wao wa siku zijazo. Kuwa na mataifa mawili.”

Ingawa Hamas wamedhoofishwa, hawajafikia kiwango cha nguvu iliyotumiwa na Israel ”kuwaangamiza”. Kwa njia moja au nyingine, Israel huenda ikalazimika kukabiliana nao kwa muda kuliko ilivyotarajia.

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *