Jobe Bellingham

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wanataka kufanya uhamisho wa mkopo wa kiungo Muingereza mwenye umri wa miaka 20 wa Borussia Dortmund, Jobe Bellingham, mwezi Januari. (Express)

West Ham na Sevilla wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Joshua Zirkzee, mwenye umri wa miaka 24, ambaye hana nafasi kikosini. (Mirror)

Manchester City, Manchester United na Tottenham zinaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Sporting na timu ya taifa ya Denmark, Morten Hjulmand, mwenye umri wa miaka 26. (Record)

Liverpool wanatafakari uhamisho wa washambuliaji wawili: Anthony Gordon wa Newcastle na timu ya taifa ya Uingereza, mwenye umri wa miaka 24, na Antoine Semenyo wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)

Antoine Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham na Manchester City wanamfuatilia beki wa Aston Villa na timu ya taifa ya Uingereza, Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia amekuwa akifuatiliwa na Chelsea, Liverpool, na Manchester United katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. (TBR Football)

Newcastle, Brighton, Fulham, na Brentford wanaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Middlesbrough na timu ya taifa ya vijana ya Uingereza chini ya miaka 21, Hayden Hackney, mwenye umri wa miaka 23. (TBR Football)

Roma wanataka kujadili upya masharti ya mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson, mwenye umri wa miaka 21, ambaye anaweza kurejea Brighton mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport via Sport Witness)

Mason Greenwood

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle na Tottenham wanaonyesha nia ya kumsajili beki wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Pierre Kalulu, mwenye umri wa miaka 25. (TuttoJuve)

Wafuatiliaji vipaji wa Barcelona wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Marseille na Muingereza mwenye umri wa miaka 24, Mason Greenwood. (Sun)

Inter Milan wako tayari kukubali ofa kwa kiungo wa timu ya taifa ya Poland, Piotr Zielinski, mwenye umri wa miaka 31, anayesakwa na Leeds, hivyo anaweza kuondoka mwezi Januari. (Football Insider)

Wasaka vipaji wa Arsenal, Chelsea, na Manchester City wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji chipukizi wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Lennart Karl, mwenye umri wa miaka 17. (Caught Offside)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *