
Donald Trump ametangaza kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya Thailand na Cambodia alipowasili Malaysia siku ya Jumapili kama sehemu ya ziara yake barani Asia, ziara ya kwanza tangu arudi madarakani mwezi Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkataba huo ulisainiwa Kuala Lumpur na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet na Waziri Mkuu wa Thailand Anutin Charnvirakul, pamoja na Rais wa Marekani. Donald Trump yuko katika mji mkuu wa Malaysia kwa siku hiyo kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-mashariki mwa Asia (ASEAN). Kisha atasafiri hadi Japan na Korea Kusini.
Waziri Mkuu wa Thailand Anutin Charnvirakul alichelewesha kuondoka kwake kwenda Malaysia siku ya Jumamosi, huku nchi yake ikiomboleza kifo cha Malkia Mama Sirikit, lakini alielezea nia yake ya kufanya ziara hiyo na kuomba kwamba mkataba wa amani uwasilishwe Jumapili asubuhi.
“Ili kumridhisha kila mtu kwa tukio hili kubwa, tutasaini mkataba wa amani tutakapowasili,” Trump amesema katika ujumbe uliotumwa kutoka kwa ndege ya rais kwenye jukwaa lake la Truth Social, akitoa rambirambi zake kwa “wananchi wa Thailand”, kwa kifo cha malikia wa zamani wa nchi hiyo Mama Sirikit.
Nchi hizo mbili zilipigana kwa siku tano mwezi Julai kwenye mpaka wao wanaozozania, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40 na mamia ya maelfu kuhama makazi yao katika mapigano makali zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa. Rais wa Marekani alishiriki katika mazungumzo yaliyofanya kusitisha mapigano kati ya Bangkok na Phnom Penh.