Baadhi ya wavuvi Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameahidi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Wavuvi hao wametoa ahadi hiyo kufuatia ziara iliyofanywa na mmiliki wa kambi za Interpol, Seleman Charles, katika kambi za Chamagati na Soswa.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuwahamasisha wavuvi kuhakikisha wanajitokeza mapema Oktoba 28 kuondoka kwenye kambi zao kuelekea katika vituo vyao vya kupigia kura walipojiandikisha.
Seleman Charles amewataka wavuvi hao kutumia nafasi hiyo muhimu kuchagua viongozi wanaowajali na wanaoweza kusimamia maendeleo ya sekta ya uvuvi na huduma za kijamii katika maeneo yao.
Baadhi ya wavuvi walioungana na kampeni hiyo wamesema wako tayari kushiriki uchaguzi huo kwa amani na utulivu, wakisisitiza kuwa ni wajibu wa kila raia kuhakikisha anashiriki katika mchakato wa kidemokrasia.
#StarTvUpdate
