#CAFWomensChampionsLeague: “Tarehe tisa JKT Queens wataanza kupeperusha bendera ya CECAFA”
Mlezi wa timu za JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena ametoa ratiba ya JKT Queens katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake ambapo wataanza harakati zao kucheza dhidi ya Gaborone United ya Botswana Novemba 9, 2025.
JKT Queens itashuka tena dimbani Novemba 12, kucheza dhidi ya Asec Mimosas na kisha kumaliza michezo ya hatua ya makundi kucheza dhidi ya TP Mazembe, Novemba 15.
Brigedia Jenerali Mabena ameyasema hayo leo baada ya kushuhudia droo ya kupanga makundi ambapo JKT Queens imepangwa kundi ‘B’ ikiwa pamoja na Gaborone United kutoka Botswana, Asec Mimosas kutoka Ivory Coast na TP Mazembe kutoka DR Congo.
#CAFWomensChampionsLeague