Takriban watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano mjini Douala nchini Cameroon siku ya Jumapili wakilalamikia wizi wa kura, huku raia wakizidi kusubiri matokeo ya urais baada ya uchaguzi wa Octoba 12.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Issa Tchiroma, ambaye alikuwa mgombea mkuu katika uchaguzi wa wiki mbili zilizopita dhidi ya rais ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu Rais Paul Biya aliitisha maandamano licha ya tume ya uchaguzi nchini humo kusema kuwa itatangaza matokeo kamili Jumatatu ya leo.

Tchiroma anasema alipata asilimia 54.8 ya kura, lakini wachambuzi wengi wanatarajia Biya mwenye umri wa miaka 92 kushinda muhula wa nane katika mfumo ambao wakosoaji wake wanasema umekuwa na dosari.

Rais Paul Biya anatarajiwa kuibuka mshindi katika uchaguzi huo unaopingwa na wapinzani.
Rais Paul Biya anatarajiwa kuibuka mshindi katika uchaguzi huo unaopingwa na wapinzani. REUTERS – Zohra Bensemra

Tchiroma, amabye ni waziri wa zamani na wakati mmoja akiwa mshirika mkuu rais Biya, alitofautiana na kiongozi huyo na kuamua kuwania urais dhidi yake.

Jijini Douala, gavana wa mkoa amesema kuwa waandamanaji walishambulia kikosi cha askari wa jeshi na vituo vya polisi katika wilaya mbili siku ya Jumapili hali ambayo ilisababisha vifo vya watu wanne na maafisa wa polisi kujeruhiwa.

Aidha maandamano yameshuhudiwa katika miji mingine kama vile Yaounde, Maroua, na Bafoussam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *