JEMEDARI ATOA NENO MICHUANO YA CAF:  Mchambuzi wa soka Tanzania Jemedari Said Kazumari ameitaja serikali ya Rais Samia Suluhu Ha...

JEMEDARI ATOA NENO MICHUANO YA CAF: Mchambuzi wa soka Tanzania Jemedari Said Kazumari ameitaja serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ni chachu ya mafanikio ya soka la Tanzania hasa kwa ngazi ya klabu kwa kuzishika mkono na kuandika historia ya timu nne kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya CAF.

Klabu hizo ni Simba SC na Yanga SC ambazo zipo Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam FC na Singida BS zikiwa Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ilicheza dhidi ya Nsingizini Hostpurs, Yanga ikicheza dhidi ya Silver Strikers.

Azam FC ilicheza dhidi ya KMKM na Singida BS ikicheza dhidi ya Flambeau du Centre.

#CAFCL #CAFCC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *