Makarani wa uchaguzi mkoani Tabora wametakia kujiepusha kuwa chanzo cha malalamiko wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyik…Makarani wa uchaguzi mkoani Tabora wametakia kujiepusha kuwa chanzo cha malalamiko wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyik…

Makarani wa uchaguzi mkoani Tabora wametakia kujiepusha kuwa chanzo cha malalamiko wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumatano Oktoba 29,2025.

Jumla ya makalani 824 kwenye vituo vya kura 764 katika kata 30 za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamepewa mafunzo ya namna ya bora usimamizi kwa wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura ikiwa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo hayo, Dkt Kija Maige amewataka Makarani hao kufuata sheria kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepukana na misunguano baina yao na Vvongozi wa vyama vya kisiasa na kusababisha dosari katika mchakato wa uchaguzi.

Dkt Maige amesema hayo mara baada ya makarani hao kula kiapo cha utii na uwaminifu pamoja na kujivua uanachama wa vyama vya siasa ili kusimamia kwa kufuata sheria na kanuni za tume huru ya taifa ya uchaguzi .
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *