MTANGAZAJI HINJO AFUNGUKA KUHUSU KAZI YAKE: Mtangazaji wa soka ambaye alitangaza mechi za Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa juma lililopita, Ayubu Hinjo @hinjojr afunguka mengi kuhusu namna alivyoyatekeleza majukumu yake bila kutetereka.
Hinjo alitangaza mechi kati ya Azam FC dhidi ya KMKM na mechi kati ya Singida BS dhidi ya Flambeau du Centre.
Mtangazaji huyo ametangaza jumla ya magoli 11 katika mechi hizo mbili, asema sauti yake haijatetereka na amefunguka namna anavyoitunza sauti yake.
Hinjo ametaja goli lililomvutia zaidi kati ya hayo 11 aliyoyatangaza kwenye michuano hiyo.
Hinjo amepiga stori na mtangazaji @allymufti_tz
#CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika #AyubuHinjo #Hinjo