SIMBA SC: “….ni miongoni mwa timu tatu Afrika ambazo zimefuzu mara saba mfululizo hatua ya makundi ya michuano ya CAF
Simba SC yatambia rekodi ya kuwa timu pekee Tanzania ambayo imecheza mara tano hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndani ya kipindi cha miaka saba.
Huyu hapa Ahmed Ally ambaye anasema bado hawajaridhika na malengo yao msimu huu ni kuvunja rekodi yao wenyewe ya kuishia robo fainali.
Ahmed anasema wanasubiri droo ya makundi ifanyike ili wawajue wapinzani wao, kisha wachore ramani ya kuelekea kwenye malengo yao…
#SimbaSC #AhmedAlly #CAFCL