*Dkt Samia: Mapambano ya rMgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amehitimisha kampeni zake, …*Dkt Samia: Mapambano ya rMgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amehitimisha kampeni zake, …

*Dkt Samia: Mapambano ya rMgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amehitimisha kampeni zake, huku akiahidi mapambano dhidi ya rushwa ni miongoni mwa mambo atakayoyapa uzito wa pekee.

Dkt Samia ameeleza hayo leo, Jumanne Oktoba 28, 2025, alipozungumza katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza, wakati wa hafla ya kuhitimisha kampeni zake za urais.

Amesema atakapopewa ridhaa ya kuiongoza nchi, atasimamia vita dhidi ya rushwa, licha ya hatua kubwa iliyopigwa na Tanzania katika kudhibiti vitendoi hivyo.

“Kama mnavyojua kwa kiasi fulani Tanzania tumepanda kwenye kutokuendekeza rushwa, tumeachana na mambo ya rushwa na hadhi yetu inapanda polepole kwa hiyo tutaendelea na kazi hiyo,” amesema.

Eneo lingine atakalolipa mkazo wa pekee, amesema ni maridhiano, utawala bora na upatikanaji wa katiba mpya n ahata kulinda mil ana desturi za Mtanzania.

“Maeneo haya yana umuhimu wa pekee katika ustawi wa Taifa na watu wake. Maendeleo jumuishi tunayokusudia hayana budi kuendana na falsafa yetu ya R4,” amesema.

Amesema amedhamiria kwa dhati kuanzisha tume ya upatanishi ili kujenga msingi wa umoja wa kitaifa, huku akitarajia kupewa imani ili kuwalipa uadilifu na ufanisi katika kuitumikia nchi na kustawisha utu wa Mtanzania.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *