KARIA ATAKA WATANGAZAJI WA LUGHA YA KIFARANSA: “Ligi ya Tanzania ni ligi ya Afrika”
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa amesema sasa ligi ya soka ya Tanzania imekuwa ikiwavutia wachezaji wengi wa Afrika hasa wale wanaonyanyukia, wakijua kwamba kucheza nchini itawasaidia kusonga mbele zaidi ikiwemo kufika Ulaya.
Karia ameipongeza #AzamTV ambayo inaifanya ligi kuonekana duniani kupitia #AzamMaxApp na kuongeza kuwa atazungumza na chombo hicho cha habari kuona kama itawezekana kuwa na watangazaji wa lugha ya Kifaransa pia ili mambo yawe mazuri zaidi kimataifa.
Karia amewapongeza wachezaji wa kitanzania ambao wamekuwa wakipambana mbele ya wachezaji wageni na baadhi yao wakiwaweka benchi.
Rais Karia amefanya mahojiano maalumu na @allymufti_tz
#RaisKaria #TFF #AzamTV