#KufuzuWAFCON2026 TANZANIA YAFUZU TENA WAFCON
Timu ya taifa ya Tanzania Wanawake (Twiga Stars) imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (WAFCON 2026) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Twiga Stars imefuzu baada ya kuitupa nje Ethiopia kwa jumla ya magoli 3-0 kufuatia ushindi wa 1-0 iliyoupata leo ugenini katika mchezo wa marudiano…
Goli limefungwa na Diana Lucas Msewa dakika ya 17.
FT: Ethiopia 0-1 Tanzania (Agg: 0-3)
#WAFCONQualifiers #KufuzuWAFCON #WAFCONQ #TwigaStars #Ethiopia #EthiopiaTanzania

