Maandalizi ya upigaji kura mkoani Tabora yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Oktoba 29,2025 yamekamilika kwa asilimia 100Maandalizi ya upigaji kura mkoani Tabora yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Oktoba 29,2025 yamekamilika kwa asilimia 100

Maandalizi ya upigaji kura mkoani Tabora yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Oktoba 29,2025 yamekamilika kwa asilimia 100.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Tabora, Elihuruma Nyella amesema vifaa vyote vya kupigia kura vimeshawasili katika vituo husika na watendaji kwenye mafunzo maalum wameanza kuelekea vituoni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya zoezi la kupiga kura.

Amesema , Mkoa wa Tabora una jumla ya wapiga kura 1,799,000 walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, ambao wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo kupitia vituo 4,724 vilivyotayarishwa katika maeneo mbalimbali.

Ameomgeza kuwa maandalizi hayo yanatoa taswira kwamba Mkoa wa Tabora uko tayari kikamilifu kwa ajili ya zoezi la kupiga kura kesho ambao hali ya usalama ikiripotiwa kuwa shwari.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *