Mpiga kura akipigwa picha

Upigaji wa kura ni hatua ya msingi katika mfumo wa kidemokrasia. Kila raia mwenye umri wenye sifa za kikatiba ana haki ya kushiriki katika uchaguzi, na kila kura inahesabiwa kwa usawa.

Kuelewa kura ni jukumu muhimu kwa kila raia katika mfumo wa kidemokrasia. Uelewa huu unamwezesha mpiga kura kufanya maamuzi sahihi yanayoakisi mahitaji na matarajio ya jamii yake.

Raia anapojua maana ya kura yake, anachangia katika uongozi bora na uwajibikaji wa serikali.

Ni nani anayeruhusiwa kupiga kura?

ili mtu aweze kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

  • Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
  • Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura
  • Awe amejiandikisha katika Jimbo au Kata; na
  • Awe katika kituo alichopangiwa katika eneo la uchaguzi ambalo amejiandikisha kama mpiga kura.

Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani inamruhusu mtu kupiga kura kwa kufuata utaratibu ufautao:

  • Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake ya kupigia kura.
  • Mpiga kura anatakiwa kupanga mstari akiwa kituo cha kupigia kura na kusubiri hadi zamu yake ya kupiga kura itakapowadia.
  • Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni.
  • Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani.
Unaweza kusoma

Maandalizi kabla ya kupiga kura

Kabla ya kuingia kwenye kituo cha kupigia kura, raia anapaswa kuthibitisha kwamba amesajiliwa katika orodha ya wapigaji kura na kuandaa kitambulisho chake cha kigeni au kitambulisho kingine kinachokubalika kama vile;

  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA);
  • Leseni ya udereva; au
  • Pasi ya kusafiria(Passport)

Lakini kwa sharti kwamba, majina yake yaliyopo katika kitambulisho atakachowasilisha mpiga kura, ni lazima yafanane na majina yote kama yalivyo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kwa mpiga kura asiye na picha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lakini ana kadi ya Mpiga Kura yenye taarifa binafsi zilizomo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ataruhusiwa kupiga kura.

Kwa mpiga kura ambaye ameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na taarifa zake zipo katika Daftari la Kudumu la wapiga kura lililopo katika kituo husika, lakini amepoteza kadi yake au kadi yake imeharibika, ataruhusiwa kwa kutumia vitambulisho vyake.

Kuelewa kura yako;

Kwanza, ni muhimu kuelewa aina ya kura unayopiga. Kwa Tanzania, uchaguzi unaojumuisha: uchaguzi wa Rais, wabunge, na madiwani. Kila aina ya kura inahusisha chaguzi tofauti, na ni lazima kuelewa ni wagombea gani au vyama gani unavyopigia kura.

Pata taarifa rasmi: Orodha ya wagombea hutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) au mamlaka ya uchaguzi ya eneo husika.

Soma majina kwa makini: Hakikisha unawatambua wagombea wote katika nafasi husika, Rais, Mbunge, Diwani, au Viongozi wa Mitaa.

Usiangalie jina tu: Angalia pia chama cha mgombea, historia yake, na wasifu wake (elimu, kazi, na uzoefu katika uongozi au jamii).

Jinsi ya kupiga kura;

Wakati wa kupiga kura, raia anapewa karatasi ya kura, gusia pia walemavu wa macho na walemavu wa viungo wanavyopiga kura, kulingana na mfumo na sheria.

Watu wenye Ulemavu;

Kwa kuzingatia hali zao, watu wenye Ulemavu wamekuwa na ushiriki mdogo kwenye Uchaguzi Mkuu.

Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na mila potofu katika baadhi ya jamii ambazo haziwapi nafasi ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kundi hili pia linakosa nafasi ya kupata taarifa sahihi na za kutosha kuhusu michakato mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi, mfano:-

  • Kutokufahamu uwepo wa kifaa cha kupigia kura chenye maandishi ya nukta nundu kwenye vituo (tactile ballot folder).
  • Matumizi ya kituturi kwamba kinamwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.
  • Kupewa kipaumbele wafikapo vituoni.
  • Kuruhusiwa kwenda na wasaidizi wao.
  • Haki, wajibu na umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki kwenye uchaguzi.

Baada ya kupiga kura

Baada ya kupiga kura, raia anatakiwa kuondoka eneo la upigaji kura kwa utulivu,

Kila kura ina thamani na ni uwajibikaji wa kila raia kushiriki.kama hiki “Kura yako siyo tu chaguo lako, bali ni sauti yako katika kuunda mustakabali wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *