Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei ameeleza kuwa Kazem Gharibabadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amefanya ziara nchini Afghanistan ili kujadili masuala kadhaa ambayo yamesalia kwenye ajenda ya uhusiano kati ya nchi mbili, ikiwa ni pamoja na suala la usalama wa mipaka.

Baqaei amebainisha haya jana katika  mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari mjini Tehran siku mbili baada ya ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika nchi jirani ya Afghanistan.

Esmaeil Baqaei amewaambia waandishi wa habari kwamba: Ziara ya Gharibabadi nchini Afghanistan imefanyika kwa madhumuni ya kujadili masuala kadhaa ambayo yamesalia katika ajenda ya uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afghanistan.

Masuala haya ni pamoja na usalama wa mipaka, haki ya maji, pamoja na ushirikiano wa kisheria na mahakama. Masuala haya yote matatu yalijadiliwa hasa wakati wa vikao na maafisa husika wa Afghanistan.

Ameongeza kuwa: Kazem Gharibabadi na maafisa wa Afghanistan pia wamekubaliana kuanza tena utekelezaji wa mpango wa kukarabati alama za mpakani, ambazo zilisitishwa kwa muda mrefu. 

Maafisa wa Iran na Afghanistan pia walichunguza  njia mbalimbali za kukabiliana na machafuko ya kiholela, biashara haramu ya dawa za kulevya na magendo ya binadamu, na aina nyingine za jinai za kuratibiwa. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema anatumai kuwa  majadiliano yaliyofanywy ana maafisa wa nchi mbili yataimarisha ushirikiano kati ya pande mbili katika nyanja mbalimbali.  

Katika sehemu nyingine ya mkutano wake na waandishi wa habari, mwandishi wa habari alimuuliza.Esmail Baqaei kuhusu madai ya Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwamba mazungumzo ya nyuma ya pazia yanaendelea ili kuanza tena ukaguzi katika maeneo ya nyuklia ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alijibu kwa kusema: “Binafsi sijasikia hili kutoka kwa Bwana Grossi,” na ushirikiano wa Iran na IAEA ni kwa mujibu wa sheria iliyoidhinishwa na Bunge la Iran katika majira ya kiangazi kufuatia mashambulizi ya Juni ya Israel na Marekani katika vituo vya nyuklia vya nchi hii.”  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *