Mamilioni ya Watanzania wanapiga kura hivi leo, kuwachagua madiwani, wabunge na rais, kaika uchaguzi ambao rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushinda, kufuatia wapinzani wake wakuu kufungwa na kuzuiwa kushiriki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi, wapiga kura Milioni 37 wameandikishwa kwenye daftari la wapiga kura.

Vituo vya kupigia kura, vimefunguliwa saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa 10 na nusu jioni.

Huu ni uchaguzi unaofanyika, wakati huu wapinzani wakuu, wakiongozwa na Tundu Lissu, kutoka chama cha upinzani CHADEMA akiwa jela, ambapo amefunguliwa mashtaka ya uhaini kwa madai ya kupanga njama za kuzuia uchaguzi huu.

Chama chake, hakishiriki kwenye uchaguzi huu, kimekuwa kikishinikiza mageuzi kabla ya kufanyika kwa zoezi hili, na hivyo hakikutia saini maadili ya uchaguzi na hivy kufungiwa nje.

Mpinzani mwingine, alionekana kuleta ushindani, ni Luhaga Mpina kutoka chama cha ACT-Wazalendo, yeyé alizuiwa na Tume ya Uchaguzi kushiriki na kupoteza kesi ya kupinga maamuzi haya.

Aidha, kuelekea uchaguzi huu mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International, yaliyoshtumu Tanzania kwa kuwatisha wakosoaji wake na hata kuwezesha matukio ya utekaji, madai ambayo serikali ya Tanznaia inakanusha.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanasema, uchaguzi huu ni muhimu kwa rais Samia, mwanamke wa kwanza kuongoza Tanzania, kuendeleza uongozi wake kwa miaka mitano ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *