Wakazi wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia elimu ya ufundi stadi (VETA) ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi nyumba iliyounganishwa umeme kupitia programu ya Wanawake na Samia kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Mkinga, Katibu Tawala Wilaya wa wilaya hiyo Mwanamwaya Kombo amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya mabadiliko hususani kwa wanawake wengi katika kupata ujuzi na ufundi vitu mbalimbali
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Mkinga, Kelvin Haule, amesema chuo hicho kipo katika mchakato wa kuanzisha programu mpya zinazolenga kuendana na shughuli za kiuchumi za eneo hilo.
Chuo Cha VETA Wilaya ya Mkinga kinauwezo wa kudahili wananfunzi 240 katika kozi za muda mrefu na Wanafunzi 100 wa kozi za muda mfupi.
#StarTvUpdates
