Ndege ya Simorgh iliyotengenezwa Iran imeanza rasmi safari zake za majaribio huku ikijiandaa kujiunga na sekta ya usafirishaji mizigo hapa nchini.

Safari za majaribio za Simorgh zilianza katika uwanja wa ndege huko Shahin Shahr katikati mwa Iran siku ya Jumanne baada ya sherehe iliyohudhuriwa na manaibu wakuu wa wizara ya ulinzi na uchukuzi ya Iran.

Shirika la Usafiri wa Anga la Iran (CAA) limeripoti kuwa, ndege hiyo inapaswa kufanya majaribio ya saa 100 ya safari za ndege katika hali mbalimbali ili kupata kibali cha mwisho cha kujiunga na sekta ya usafirishaji wa anga ya Iran.

Mkuu wa CAA, Hossein Pourfarzaneh alisema Jumanne kwamba Simorgh, ambayo mchakato wake wa uasili unfanyika kwa zaidi ya miaka 15, inaiorodhesha Iran miongoni mwa nchi zisizozidi 20 duniani zenye uwezo wa kubuni na kutengeneza ndege.

Simorgh, iliyepewa jina la ndege anayetajwa katika hadithi na fasihi ya Kiajemi, ina injini mbili zenye horsepower 2,500 ambazo zinaweza kubeba tani 6 za mizigo kwa umbali wa kilomita 3,900.

Ndege hiyo ilifanya jaribio la teksi ya haraka mnamo Mei 2022, kabla ya kufanya safari yake ya kwanza.

Ndege ya Simorgh iliyotengenezwa na wataalamu wa Iran

Simorgh imeelezwa kama ndege nyepesi, yenye kasi na uwezo mkubwa wa kubeba mizigo ambayo inaendana na hali ya hewa ya Iran, na kuifanya kuwa chaguo bora kwa huduma muhimu kama vile safari za ndege za kimatibabu.

Wataalamu pia wanaamini kwamba Simorgh inaweza kujiunga na ndege za abiria za masafa mafupi za Iran katika siku zijazo.

Ripoti katika miaka ya hivi karibuni zimeashiria mafanikio makubwa katika sekta ya uzalishaji na utengenezaji wa ndege nchini Iran.

Mafanikio haya yamepatikana licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambavyo vinazuia mashirika ya ndege nchini kununua ndege mpya au vipuri vya ndege.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *