Joshua Zirkzee

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Roma ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, kutoka Manchester United mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Crystal Palace wanafikiria kumsajili mlinzi wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 30, msimu ujao. (Teamtalk)

Ofa ya Ligi ya Saudia kwa mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 33, bado ipo mezani. (TBR Football)

Tottenham wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa West Ham wa Uingereza Jarrod Bowen, 28. (Fichajes – kwa Kihispania)

Fabio Carvalho yuko tayari kufanya mazungumzo na Brentford kuhusu mustakabali wake huku winga huyo wa Ureno, 23, akiwa mbioni kukihama klabu hicho mwezi Januari. (Sky Sports)

Chelsea wana mpango kumtema meneja Enzo Maresca na badalayake kumsajili mkufunzi wa Bournemouth Andoni Iraola. (Caught Offside)

Lyon inajilianakuhusu mpanfo wa kumsajili mshambuliaji wa Brazil Endrick, 19, kwa mkopo wa miezi sita kutoka Real Madrid mwezi Januari. (Mail)

Mshambulizi wa Brazil Neymar anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa muda mfupi na klabu ya Santos baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kuonyesha nia ya kurejea Ulaya kabla ya Kombe la Dunia mwaka ujao. (AS – kwa Kihispania)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *