.

Chanzo cha picha, Reuters

Rais wa
Marekani Donald Trump, kabla ya mkutano wake na Rais wa China Xi
Jinping siku ya Alhamisi, alisema ameiagiza Wizara ya Ulinzi kuanza mara moja
kufanya majaribio ya silaha za nyuklia “sawa sawa” na silaha zingine zenye
nguvu.

“Kwa
sababu ya programu za majaribio za nchi zingine, nimeagiza Idara ya Ulinzi
kuanza kujaribu silaha zetu za nyuklia.

Mchakato huo
utaanza mara moja,” Trump alisema kwenye mtandao wa Truth Social, kabla ya
mkutano na Xi huko Korea Kusini.

“Urusi
ni ya pili, na China ni ya tatu, lakini zitakuwa sana hata ndani ya miaka
5,” Trump alibainisha.

Rais Vladmir
Putin alisema siku ya Jumatano Urusi imefanikiwa kufanyia majaribio ndege
aina ya Poseidon super torpedo ambayo wachambuzi wa kijeshi wanasema inaweza
kuharibu maeneo ya pwani kwa kusababisha mafuriko makubwa ya bahari yenye
mionzi.

Huku Trump
akiimarisha matamshi yake na msimamo wake kuhusu Urusi, Putin ameweka hadharani
nguvu yake ya nyuklia kwa kufanya majaribio ya kombora jipya la Burevestnik
Oktoba 21 na mazoezi ya kurusha nyuklia Oktoba 22.

Marekani ilifanyia
majaribio silaha za nyuklia mara ya mwisho mwaka 1992.

Majaribio
hutoa ushahidi wa kile ambacho silaha yoyote mpya ya nyuklia itafanya – na
ikiwa silaha za zamani bado zinafanya kazi.

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *