Wabunge wa umoja wa Ulaya, hapo jana jioni walitoa tamko la Pamoja kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania waliosema haukuwa huru wala wa haki, wakizitaka nchi washirika na wadau wa demokrasia kukemea kilichofanyika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Ulaya, David McAllister, kile kilichopaswa kuonekana kama kusherehekea demokrasia, kiligeuka kuwa vitisho, hofu na ukandamizwaji wa haki za watu.

McAllister kwenye taarifa yake ameongeza kuwa uchaguzi uliofanyika hapo jana haupaswi kutambuliwa kama uchaguzi huru na haki, kwakuwa udanganyifu haukuanzia kwenye sanduku la kura peke yake bali ulianza miezi kadhaa nyuma.

Taarifa yao imeongeza kuwa, kunyanyaswa na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani, baadhi kuzuiwa kushiriki uchaguzi Pamoja na kuminywa kwa uhuru wa maoni, vimetosha kuthibitisha kuwa hakukuwa na uchaguzi wa haki.

Wabunge hao wametolea mfano kuendelea kuzuiliwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, Tundu Lissu kwa kesi waliyodai imechochewa kisiasa, kunadhihirisha nia mbaya dhidi ya wakosoaji, sasa wakitaka kiongozi huyo kuachiwa bila masharti.

Bunge hilo likitoa wito kwa washirika kusimama imara katika kutetea demokrasia na haki za binadamu, wabunge hao wakidai kukaa kimya sio kuonesha haufungamani na upande wowote bali ni kuwa mshirika wa ukatili.

Kauli ya wabunge hawa imekuja siku chache kupita tangu Serikali ya Tanzania, itupilie mbali madai yaliyotolewa na mashirika kadhaa ya kutetea kutetea haki za binadamu, yaliyoutuhumu utawala war ais Samia Kukithiri wa vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *