
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepata ushindi wa kishindo kwa kupata asilimia zaidi ya 98 ya kura, tume ya uchaguzi imetangaza leo Jumamosi asubuhi.
“Namtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,” mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jacobs Mwambegele alisema kupitia televisheni ya taifa.
Mwenyekiti wa INEC, Jacobs Mwambegele amesema kuwa Samia Suluhu Hassan ameibuka Mshindi kwa kupata 31,913,866 kati ya 32,678,844 zilizopigwa.