Inter Milan wanajiunga na wanaomwinda beki Marc Guehi, Everton inamfuatilia mshambuliaji Nicolas Jackson, na Manchester United wanakabiliwa na ushindani wa kumpata Ayyoub Bouaddi.
Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan wanataka kumsajili beki wa kati wa England Marc Guehi, 25, mkataba wake wa Crystal Palace utakapomalizika msimu ujao, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona, Bayern Munich, Real Madrid na Liverpool. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Everton inamfuatilia mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, huku Bayern Munich wakionekana kutokuwa na uwezekano wa kuanzisha uhamisho wa pauni milioni 70 kwa mshambuliaji huyo wa Chelsea anayecheza kwa mkopo. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Andrey Santos, 21, huku wakipania kuimarisha safu yao ya kiungo wa kati mwezi Januari. (Football Insider)
Kocha Ruben Amorim anatarajia baadhi ya kikosi chake cha Manchester United kuomba kuondoka Januari. (Times – subscription required)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United imekuwa na majadiliano ya ndani kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Ayyoub Bouaddi, 18. (Caught Offside)
Arsenal na Liverpool pia wako kwenye mchanganyiko wa kumsajili kijana mwenye kipaji Bouaddi. (TBR Football)
Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25, anasema hajasahau uvumi kuhusu mustakabali wake, lakini anafurahi kubaki na Cherries majira ya joto. (Sky Sports)
Ismael Saibari wa PSV Eindhoven anatarajiwa kuwindwa Januari na vilabu vingi vya Ligi ya Primia, huku Aston Villa na Leeds zikiwa miongoni mwa wale wanaomtaka kiungo huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 24. (TBR Football)
Real Madrid wameungana na Manchester United na Chelsea kumfuatilia winga wa Red Bull Salzburg wa Bosnia-Herzegovina Kerim Alajbegovic, 18. (Defensa Central – in Spanish)