Chanzo cha picha, Reuters
-
- Author, Yusuf Jumah
- Nafasi, BBC Swahili
Msimu wa uchaguzi wa Tanzania wa 2025 ulijitokeza kama dhoruba ya kisiasa iliyodhihirishwa na hofu, kuzimwa kwa sauti za wapinzani na ukosefu wa imani katika mchakato mzima wa kidemokrasia.
Kuanzia kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Tundu Lissu hadi ushindi unaopingwa wa Samia Suluhu Hassan, ambaye ametangazwa mshindi kwa takriban 98% ya kura – 31,913,866 kati ya kura 32,678,844 zilizopigwa, soma kuhusu matukio muhimu yaliyoibua kipindi kibaya cha machafuko ya hivi karibuni katika historia ya nchi hiyo .
Aprili 9: Kukamatwa kwa Tundu Lissu
Chanzo cha picha, Getty Images
Hali ya uchafuzi wa mazingira ya kisiasa ilianza wakati Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, alipokamatwa wakati wa mkutano wa kisiasa. Kuzuiliwa kwake kulileta mshtuko nchini kote, kuashiria msimamo mkali dhidi ya upinzani.
Aprili 10: Mashtaka ya Uhaini yafunguliwa
Chanzo cha picha, Getty Images
Siku moja tu baadaye, Lissu alifunguliwa mashtaka rasmi ya uhaini-kosa lisilokuwa na dhamana. Hatua hii ilimuondoa mpinzani mkuu wa chama tawala kutoka kwa kinyang’anyiro cha urais.Mawakili wake baadaye walijaribu kutafuta msaada wa mashirika makuu kama vile Umoja wa Mataifa kuitilia shinikizo serikali kumwachilia huru
Oktoba 6: Humphrey Polepole atekwa nyara
Chanzo cha picha, The Citizen
Oktoba 22: Pigo jingine kwa upinzani
Chanzo cha picha, Facebook/Heche
Oktoba 29: Siku ya Uchaguzi yageuka kuwa na vurugu
Chanzo cha picha, Reuters
Oktoba 30: Jeshi latoa onyo
Chanzo cha picha, Getty Images
Novemba 1: Samia Suluhu atangazwa mshindi
Chanzo cha picha, SCREENGRAB/TBC TANZANIA
Matokeo hayo yaliyotangazwa na INEC yanampa Samia Suluhu Hassan fusra ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Samia Suluhu Hassan ameweka historia nchini Tanzania kwa kuwa Rais Wa Kike Wa Kwanza aliyechaguliwa .
Uchambuzi: Ni nini sasa mustakabali wa Tanzania?
Chanzo cha picha, Reuters
Uchaguzi wa 2025 umeiacha Tanzania katika njia panda. Mkono mzito wa serikali katika kukabilina na upinzani na kutengwa kwa vyama vikuu vya upinzani kumezua wasiwasi mkubwa juu ya kurudi nyuma kwa demokrasia. Wachambuzi wanaonya kuwa:
• Mgawanyiko wa Kisiasa Utazidi Kuongezeka: Mbinu za ukamataji na vitisho zimeondoa imani katika taasisi za serikali, na kufanya maridhiano kuwa magumu zaidi.
• Nchi kuangaziwa/Kutazamwa kwa karibu zaidi Kimataifa: Makundi ya haki za binadamu na serikali za kigeni zinaweza kushinikiza uwajibikaji, uwezekano wa kuathiri misaada na uhusiano wa kidiplomasia.
• Uthabiti wa Kiuchumi upo hatarni: Machafuko ya muda mrefu na kutokuwa na uthabiti wa kisiasa unaweza kuzuia uwekezaji na kuzorotesha uchumi ambao tayari unakabiliana na mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira.
• Kujipanga upya kwa Upinzani: Licha ya ukandamizaji, vuguvugu la upinzani linaweza kujipanga upya kwa siri au kutafuta ushirikiano mpya na hivyo kuweka mazingira ya makabiliano katika siku zijazo.
• Mwanzo mpya : Licha ya hali ya wasi wasi iliyopo sasa ,pia kuna uwezekano wa awamu hii ya historia ya Tanzania ikachangia hatua kama ushirikiano kati ya serikali na upinzani kuleta marekebisho katika taasisi kama vile tume ya uchaguzi na hata katiba mpya na kukomeshwa kwa ukandamazaji wa wapinzani na uhuru zaidi wa kujieleza na wa vyombo vya habari.
Kwa Watanzania wa kawaida, swali linabaki: Je, miaka mitano ijayo italeta utulivu na mageuzi au misukosuko zaidi?