
Rais Mteule Samia Suluhu Hassan ametoa hotuba yake ya kwanza baada ya kupewa cheti cha ushindi kwenye uchaguzi wa 2025.
“Chama cha Mapinduzi kupitia mimi, Tumepokea cheti hiki cha Ushindi cha Uchaguzi Mkuu heshima na Unyenyekevu mkubwa sana. Cheti hiki ni uthibitisho wa Imani ya wananchi kunikabidhi mimi na chama cha Mapinduzi dhamana ya kwenda kutekeleza ahadi yetu ya kuimarisha kuilinda na kuijengea heshima na utu wa Mtanzania.”
Rais Samia akizungumza katika hotuba yake, alisema kuwa ni Uchaguzi wa 2025, ni wa kwanza katika historia kufanyika nchini humo kwa nguvu yao wenye, “kwa raslimali zetu wenyewe” na pia kuwa kati ya wagombea 17, wanne ni wanawake.