Chanzo cha picha, Rex Features
Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 65msimu ujao na mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 32 anatathmini chaguo alizo nazo ikiwa ni pamoja nakusalia Ujerumani au kuhamia Barcelona. (Sport – kwa Kihispania)
Manchester United na Tottenham wanamfuatilia kwa karibu beki wa England Jarrad Branthwaite, 23, ambaye Everton hawana mpango wa kumuuza. (Caught Offside)
Tottenham na Chelsea wanatarajiwa kumenyana katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Porto Mhispania Samu Aghehowa, 21, ambaye anaweza kupatikana kwa euro 80m (£70.5m). (Correio da Manha via Goli)
Arsenal na Barcelona wanamfuatilia nahodha wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 16, Lacine Megnan-Pave baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kufunga mabao 15 na kusaidia kufunga mabao12 katika mechi 24 katika timu ya wachezaji wa Montpellier walio chini ya umri wa miaka 17. (Sport – kwa Kihispania)
Msaka vipaji mkuu wa Liverpool Barry Hunter alikuwa Craven Cottage Jumamosi kufuatilia usajili wa Fulham majira ya joto wa pauni milioni 35, winga wa Brazil Kevin, 22, katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Wolves. (Football Insider)
Meneja wa Bournemouth Andoni Iraola anapigiwa upatu kujiunga na Athletic Club ikiwa Ernesto Valverde hatakubali kuongeza mkataba wake nao msimu ujao (La Razon – kwa Kihispania)