Kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo akiwa amevalia sare za kijeshi na miwani nyeusi

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

    • Author, Alex de Waal
    • Nafasi, Mchambuzi wa Afrika

Mohamed Hamdan Dagolo, anayefahamika kama “Hemedti”, ameibuka kuwa kiungo muhimu katika jukwa la kisiasa la Sudan, kikosi chake cha Rapid Support Forces (RSF) sasa kikiongoza nusu ya nchi hiyo.

RSF ilipata ushindi mkubwa hivi karibuni wakati ilipochukua udhibiti wa mji wa el-Fasher, ambao ulikuwa kambi ya mwisho kushikiliwa na jeshi la sudana na washirika wake katika eneo la magharibi la Dafur.

Japo anaogopwa na kuchukiwa na mahasimu wake, Hemedti anapendwa na wafuasi wake kwa ukakamavu wake, ukatili, na ahadi yake ya kukomeshi hali ya taifa iliyodharauliwa.

Hemedti alikulia katika katika mazingira ya kawaida tu. Familia yake inatoka sehemu ya Mahariya ya jamii Rizeigat ambayo ni ya wafugaji wa ngamia, wanaozungumza Kiarabu na wanapatikana Chad na Darfur.

Alizaliwa mwaka wa 1974 au 1975 – kama wakaazi wengi wa vijijini, tarehe yake ya kuzaliwa na mahali alipozaliwa haikunakiliwa.

Wakiongozwa na mjomba wake Juma Dagolo, ukoo wake ulihamia Darfur katika miaka ya 1970 na 80, wakikimbia vita na kutafuta malisho na makaazi.

Baada ya kuacha shule akiwa mdogo, Hemedti alipata pesa za biashara ya ngamia kutoka jangwani hadi Libya na Misri.

Wakati huo, Darfur ilikuwa magharibi mwa Sudan – eneo masikini lililokumbwa na vurugu ambalo lilitelekezwana serikali ya Rais wa wakati huo Omar al-Bashir.

Wanamgambo wa kiarabu waliojulikana kama Janjaweed – waliojumuisha kikosi kilichoongozwa na Juma Dagolo – walikuwa wakishambulia vijiji vya wazaliwa wa jamii ya Fur.

Mzunguko huo wa ghasia ulisababisha uasi kamili mwaka 2003, ambapo wapiganaji wa Fur waliungana na Masalit, Zaghawa na makundi mengine, wakisema walikuwa wamepuuzwa na viongozi wa Kiarabu wa nchi hiyo.

Kwa kujibu hatua hiyo, Bashir aliiwezesha sana Janjaweed na kuipatia jukumu la kuongoza juhudi zake za kukabiliana na uasi. Haikuchukua muda kundi hilo likapata umaarufu kwa kuchoma, kupora, kubaka na kuua.

Mpiganaji wa waasi wa Sudan akitazama kijiji cha Chero Kasi kilichotelekezwa chini ya saa moja baada ya wanamgambo wa Janjaweed kukivamia katika ghasia zilizokumba jimbo la Darfur tarehe 7 Septemba 2004.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kikosi cha Hemedti kilikuwa miongoni mwao, ripoti ya Walinda Amani wa Umoja wa Afrika wakisema kilishambulia na kuharibu kijiji cha Adwa mwezi Novemba 2004, na kuwaua watu 126 people, wakiwemo watoto 36.

Uchunguzi wa Marekani ulibaini kuwa Janjaweed walifanya mauaji ya halaiki.

Mzozo wa Darfur ulipelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo iliwafungulia mashtaka wanaume wanne, akiwemo Bashir, ambaye amekana kutekeleza mauaji ya kimbari.

Hemedti alikuwa mmoja wa makamanda kadhaa wa Janjaweed walioonekana kuwa mtu mdogo sana kuwa machoni mwa mwendesha mashtaka wakati huo.

Mmoja tu, “kanali wa makanali” wa Janjaweed, Ali Abdel Rahman Kushayb, alifikishwa mahakamani.

Mwezi uliopita alipatikana na hatia ya makosa 27 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu na hukumu dhidi yake itatolewa tarehe 19 Novemba.

Katika miaka iliyofuata kuongezeka kwa ghasia mwaka 2004, Hemedti alicheza karata zake kwa ustadi, akipanda cheo hadi kuwa mkuu wa kikosi chenye nguvu cha kijeshi, himaya ya kampuni, na uwezo wa kisiasa.

Ni hadithi ya fursa na ujasiriamali. Aliasi kwa muda mfupi, akidai malipo kwa askari wake, kupandishwa cheo na ndugu yake kupewa wadhifa wa kisiasa. Bashir alidhia sehemu kubwa ya matakwa hayo na hivyo basi Hemedti akajiunga tena na kundi hilo.

Baadaye, wakati vitengo vingine vya Janjaweed vilipoasi, Hemedti aliongoza vikosi vya serikali vilivyowashinda, katika mchakato wa kuchukua udhibiti wa mgodi mkubwa wa dhahabu wa Darfur mahali panapojulikana kama Jebel Amir.

Kwa haraka, kampuni ya familia ya Hemedti ya Al-Gunaid ikawa msafirishaji mkuu wa dhahabu wa Sudan.

Mwaka 2013, Hemedti aliomba- kupata – hadhi rasmi kama mkuu wa kundi jipya la wanamgambo, RSF, akiripoti moja kwa moja kwa Bashir.

Janjaweed ilibadilishwa jina na kuwa RSF, wakipata sare mpya, magari na silaha – na pia maafisa kutoka jeshi la kawaida ambao waliletwa kuimarisha usalama.

Mwanaume wa Sudan anapiga picha ya selfie na wanachama wa Rapid Support Forces (RSF), wakiwa na sare na bunduki, katika mji mkuu Khartoum tarehe 18 Juni 2019.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

RSF ilipata ushindi muhimu dhidi ya waasi wa Darfur, haikufanya vyema katika kupambana na uasi katika Milima ya Nuba karibu na Sudan Kusini, na ilichukua mkataba mdogo wa polisi katika mpaka na Libya.

Wakizuia uhamiaji haramu kutoka Afrika kupitia jangwa hadi Bahari ya Mediterania, makamanda wa Hemedti pia walibobea katika unyang’anyi na, inasemekana, biashara ya watu.

Mnamo mwaka wa 2015, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zilitoa wito kwa jeshi la Sudan kutuma wanajeshi kupigana dhidi ya Houthis huko Yemen.

Kikosi hicho kiliongozwa na jenerali ambaye alipigana huko Darfur, Abdel Fattah al-Burhan, ambaye sasa ni mkuu wa jeshi linalopigana na RSF.

Hemedti aliona nafasi na akafanya makubaliano tofauti, ya kibinafsi na Saudi Arabia na UAE ili kutoa mamluki wa RSF.

Muunganisho wa Abu Dhabi ulionekana kuwa muhimu zaidi. Ilikuwa mwanzo wa uhusiano wa karibu na rais wa Imarati, Mohamed bin Zayed

Vijana wa Kisudan – na kuongezeka kutoka nchi jirani pia – walitembea hadi vituo vya kuajiri vya RSF kwa malipo ya pesa taslimu ya hadi $6,000 (£4,500) wakati wa kujiandikisha.

Hemedti alianzisha ushirikiano na kampuni ya Wagner Group ya Urusi, akipokea mafunzo kwa ajili ya shughuli za kibiashara zikiwemo za dhahabu.

Alitembelea Moscow ili kurasimisha mpango huo, na alikuwepo siku ambayo Urusi iliivamia Ukraine. Baada ya vita nchini Sudan kuzuka, alikanusha RSF kupata msaada kutoka kwa Wagner.

Ingawa vitengo vikuu vya vita vya RSF vilizidi kuwa na taaluma, pia vilijumuisha muungano wa wanamgambo wa kikabila wasio wa kawaida.

Wakati serikali ikikabiliwa na maandamano ya wananchi yanayoongezeka, Bashir aliamuru vitengo vya Hemedti kwenye mji mkuu wa Khartoum.

Akitumia jina lake, rais alimuita himayti, “mlinzi wangu”, akiona RSF kama mzani dhidi ya watu wanaoweza kufanya mapinduzi katika jeshi la kawaida na usalama wa taifa.

Ilikuwa ni hesabu mbaya. Mnamo Aprili 2019, waandamanaji walizunguka makao makuu ya jeshi wakidai demokrasia.

Bashir aliamuru jeshi kuwafyatulia risasi. Majenerali wakuu – akiwemo Hemedti- walikutana na kuamua kumwondoa Bashir badala yake. Harakati za demokrasia zilipongezwa.

 Omar al-Bashir (Kushoto) waves a walking stick as he gives a speech at the headquarters of the Rapid Support Forces (RSF) paramilitaries in Umm al-Qura in South Darfur State, while RSF commander Mohamed Hamdan Daglo, wearing a cap, looks on

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Kwa mara ya kwanza, Hemedti alionekana kama sura mpya itakatoa taswira ya mustakabali wa Sudan ya siku zijazo. Akiwa kijana, mtulivu alikutana na makundi mbalimbali ya kijamii, na kujiweka kama mpinzani wa uanzishwaji wa kihistoria wa nchi, alijaribu kubadilisha misimamo yake ya kisiasa. Hali hiyo ilidumu kwa majuma machache tu.

Wakati yeye na mkuu wa pamoja wa baraza tawala la kijeshi, Burhan, walipokwama katika mzozo wa kukabidhi madaraka kwa raia, waandamanaji walizidisha mikutano yao, na hapo ndipo Hemedti alizindua RSF, ambayo iliua mamia ya watu, kuwabaka wanawake, na kuwatupa wanaume kwenye Mto Nile na matofali yamefungwa kwenye vifundo vyao vya miguu, kulingana na ripoti ya shirika la kampeni la Human Rights Watch (HRW).

Hemedti amekanusha ripoti hiyo inayomuhusisha na ukatili dhidi ya Wasuda wenzake.

Baada ya shinikizo kutoka kwa kundi la nchi zilizoundwa ili kukuza amani na demokrasia nchini Sudan – Marekani, Uingereza, Saudi Arabia na UAE – majenerali na raia walifikia mwafaka wa kisiasa uliosimamiwa na wapatanishi wa Kiafrika.

Kwa miaka miwili, kulikuwa na mshikamano utulivu japo wa kusuasua katika baraza kuu la uongozi lililoongozwa na jeshi na baraza la mawaziri la kiraia.

Wakati kamati iliyoteuliwa na baraza la mawaziri kuchunguza kampuni zinazomilikiwa na jeshi, usalama na RSF walifunga ripoti yake ya mwisho – ambayo iliwekwa kufichua jinsi Hemedti alivyokuwa akipanua himaya yake ya ushirika – Burhan na Hemedti waliwafukuza raia na kuchukua madaraka.

Hemedti alipinga. Siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya Aprili 2023 kutatua suala hili, vvikosi vya RSF vikaamua kuzingira makao makuu ya jeshi na kuteka kambi muhimu na ikulu ya kitaifa katika mji mkuu, Khartoum.

Mpango huo ulitibuka na badala na ukageuza, mji wa Khartoum kuwa uwanja la vita huku vikosi pinzani vikipambana mitaani.

Ghasia zililipuka huko Darfur, huku vikosi vya RSF vikianzisha kampeni mbaya dhidi ya watu wa Masalit.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa raia 15,000 walikufa, na Marekani ilielezea kama mauaji ya kimbari. RSF ilikanusha madai hayo.

Makamanda wa RSF walisambaza video za wapiganaji wao wakiwatesa na kuua, wakitangaza ukatili huo na hisia zao za kutokujali.

RSF na washirika wap walivamia Sudan nzima, wakipora miji, masoko, vyuo vikuu na hospitali.

Bidhaa zilizoporwa zinauzwa katika yale yanayojulikana kama “masoko ya Dagolo” yanayosambaza bidhaa kutoka Sudan hadi Chad na nchi nyingine jirani. RSF imekanusha madai ya wapiganaji wake kuhusika katika uporaji.

Akiwa amenaswa katika ikulu ya taifa chini ya mashambulizi ya mizinga na mashambulizi ya anga, Hemedti alijeruhiwa vibaya katika wiki za mwanzo za mzozo huo na kutoweka machoni pa watu.

Alipojitokeza tena miezi kadhaa baadaye hakuonyesha kujuta kwa ukatili na pia aliazimia kushinda vita kwenye uwanja wa vita.

Halima Mohammed Adam, a Sudanese cholera patient with a brown shawl over her head and wearing a multi-coloured dress, looks on as she sits on a bed at a United Nations-run makeshift clinic in Tawila in Darfur, Sudan, on 5 August 2025

Chanzo cha picha, Reuters

RSF imepata silaha za kisasa ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani za kisasa, ambazo imetumia kushambulia mji mkuu wa Port Sudan unaoshikiliw ana Burhan, na ambazo zilikuwa na jukumu muhimu katika shambulio la El-Fasher.

Ripoti za uchunguzi miongoni mwa nyinginezo, New York Times, zimeandika kwamba hizi husafirishwa kupitia uwanja wa ndege na kituo cha usambazaji kilichojengwa na UAE ndani ya Chad. UAE inakanusha kuwa inaipatia RSF silaha.

Kwa silaha hii, RSF imefungwa katika mkwamo wa kimkakati na mshirika wake wa zamani, jeshi la Sudan.

Hemedti anajaribu kubuni muungano wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya makundi ya kiraia na vuguvugu la watu wenye silaha, hasa wapinzani wake wa zamani katika Milima ya Nuba.

Ameunda “Serikali ya Amani na Umoja” sambamba na kuchukua uenyekiti kwa ajili yake.

Baada ya kuteka mji wa al-Fasher, RSF sasa inadhibiti karibu eneo lote la magharibi mwa Mto Nile.

Kufuatia kuongezeka kwa taarifa za mauaji yanayofanywa na kundi hilo na kukosolewa vikali, Hemedti alitangaza uchunguzi juu ya kile alichokiita ukiukaji uliofanywa na wapiganaji wake wakati wa kutekwa kwa El-Fasher.

Wasudan wanakisia kwamba Hemedti anajiona kama rais wa taifa lililojitenga, au bado ana nia ya kutawala Sudan yote.

Pia huenda anajiona siku kama kibaraka wa kisiasa wa siku za usoni kutokana na uwezo wake, na mkuu wa muungano unaodhibiti biashara, jeshi la mamluki na chama cha siasa. Kwa njia hizi, hata kama hakubaliki Sudan, bado anaweza kuelekaeza maamuzi yatakayofanywa nchini humo.

Na huku wanajeshi wa Hemedti wakiwaua raia huko al-Fasher, ana imani kwamba anafurahia hali ya kutokujali katika ulimwengu ambao haujali vile.

Alex de Waal ni mkurugenzi mtendaji wa Wakfu wa Amani Ulimwenguni katika Shule ya Sheria na Diplomasia ya Fletcher katika Chuo Kikuu cha Tufts nchini Marekani.

Ramani ya Sudan inayoonyesha udhibiti wa maeneo kufikia tarehe 28 Oktoba 2025. Maeneo yanayodhibitiwa na jeshi na washirika wake yametiwa alama nyekundu, RSF na washirika wake kwa rangi ya buluu, na makundi mengine yenye silaha kwa rangi ya njano. Miji muhimu kama vile Khartoum, na el-Fasher yameandikwa . Mto Nile pia umeonyeshwa. Chanzo: Critical Threats Project at the American Enterprise Institute.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *