
Israeli imetangaza kwamba vikosi vyake vya usalama vimepokea mwili wa mateka wa Gaza kutoka kwa hirika la Msalaba Mwekundu siku ya Jumanne jioni, na kurejeshwa kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas. Jeneza la mateka huyo “limekabidhiwa kwa jeshi na Shin Bet,” idara ya usalama wa ndani, na litasafirishwa nchini Israel kwa sherehe ya kijeshi na utambuzi, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema katika taarifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kikosi cha Hamas kimetangaza Jumanne, Novemba 4, kwamba kitakabidhi saa 2:00 usiku saa za Gaza mwili wa mateka aliyekamatwa mnamo Oktoba 7, 2023, na kupelekwa Gaza, kama sehemu ya mabadilishano ya mateka na wafungwa yaliyokubaliwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel, ambayo yamekuwa yakitumika tangu Oktoba 10.
Kikosi cha Ezzedine Al-Qassam “kitakabidhi mwili wa mmoja wa wafungwa wa uvamizi (Israel), ambao ulipatikana katika kitongoji cha Shuja’iyya mashariki mwa Jiji la Gaza, saa 2:00 usiku saa za Gaza,” kikosi cha Hamas kimetangaza kwenye kituo chake cha Telegram. “Tunaendelea kufanya kazi ili kukamilisha mchakato wa kukabidhi miili ya mateka wa Israel licha ya ugumu na vikwazo, na tunafanya kazi ili kukamilisha mchakato mzima wa mabadilishano haraka iwezekanavyo,” msemaji wa Hamas Hazem Qassem amesema katika taarifa tofauti.
Tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, Hamas imewaachilia mateka 20 waliosalia badala ya kuachiliwa huru kwa wafungwa wapatao 2,000 wa Kipalestina na imeanza kurudisha mabaki ya wale waliouawa.
Kati ya miili 28 husika, 20 tayari imerejeshwa, ikiwa ni pamoja na Waisraeli 18, Mthailand mmoja, na Mnepali mmoja. Mateka wanane waliofariki bado hawajarejeshwa.