Maino

Kiungo wa kati wa England Kobbie Mainoo anakaribia kuondoka Manchester United kuelekea Napoli huku juhudi za kufikia mkataba wa bila malipo kwa mchezaji huyo wa miaka 20 zikiongezwa. (Teamtalk)

Barcelona itamsijili Marcus Rashford kutoka Manchester United kwa mkataba wakudumu endapo mchezaji huyo wa kimataifa wa England atakubali pendekezo lao la mshahara. (Talksport)

Wakala Niclas Fullkrug anasema ”heri” mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 aondoke klabu ya West Ham. (TOMorrow Business Podcast via Athletic)

Mlinzi wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24, amesema ”alikamia” sana kujiunga na Real Madrid kabla ya kusaini mkataba mpya na The Gunners mwezi Septemba. (Sports Illustrated)

Idara ya usajili ya Newcastle imemtaja kiungo wa Atalanta Ederson, 24, katika mikutano ya hivi majuzi kama mrithi anayepigiwa upatu kuchukua ncafasi ya Mbrazil mwenzake Joelinton, 29. (The I)

Liverpool wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa River Plate mwenye umri wa miaka 18 kutoka Argentina Ian Subiabre. (Fichajes – kwa Kihispania)

Chelsea na Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Vitor Roque, 20, kutoka Palmeiras. (Mundo Deportivo)

Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag ni miongoni mwa makocha wanaotajwa na Wolves bila uamuzi wowote kuhusu mrithi wa Vitor Pereira kama kocha mkuu anayetarajiwa wiki hii. (Athletic – usajili unahitajika)

Kiungo wa kati wa Uhispania Oriol Romeu, 34, atajiunga tena na klabu yake ya zamani ya Southampton baada ya kukatisha mkataba wake na Barcelona. (Sport – kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 25, huenda akahamia Tottenham au Bayern Munich Januari baada ya kutatizika kutulia Juventus tangu alipohamia klabu hiyo ya Serie A msimu wa joto. (Sky Sports)

Kocha wa zamani wa Roma, Daniele de Rossi sasa ndiye mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa Genoa, baada ya Patrick Vieira kutimuliwa hivi majuzi. (Football Italia)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *