Chanzo cha picha, Getty Images
-
- Author, Anthony Zurcher
- Nafasi, Mwandisi Amerika Kaskazini
Zohran Mamdani, meya mpya wa Jiji la New York, atakuwa meya mwenye umri mdogo zaidi wa jiji hilo tangu 1892, meya wa kwanza Muislamu na meya wa kwanza kuzaliwa barani Afrika.
Aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho mwaka jana licha ya kutokuwa na jina tajika, pesa kidogo na bila uungwaji mkono wa chama.
Hilo pekee linafanya ushindi wake dhidi ya Gavana wa zamani Andrew Cuomo na mgombea mteule wa Republican Curtis Silwa kuwa wa ajabu.
Lakini zaidi ya hayo, anawakilisha aina ya mwanasiasa ambaye wengi katika chama cha mrengo wa kushoto cha Democratic wamekuwa wakimtafuta kwa miaka mingi.
Umri mdogo na haiba yake, inamfanya kuwa karibu na kizazi chake ambacho kinaongoza masuala yanayojadiliwa katika mitandao ya kijamii.
Mamdani pia ameonyesha uwezo mkubwa wa kushughulikia masuala ya kiuchumi ambayo yamekuwa kipaumbele cha wapiga kura wanaofanya kazi ambao walijitenga na chama cha Democratic hivi karibuni, lakini hajajiondoa katika kanuni za kitamaduni za mrengo huo wa kushoto.
Lakini wakosoaji wameonya kwamba mgombea kama huyo hawezi kuchaguliwa katika maeneo makubwa ya Marekani – na Republican wamechukulia ushindi wa mwanasoshalisti huyo wa chama cha Democratic kama sura mrengo wa kushoto. , Jumanne usiku huko New York City, alikuwa mshindi.
Kwa kupambana na kumshinda Cuomo, gavana wa zamani wa New York ambaye mwenyewe ni mtoto wa gavana, ameshinda uanzishwaji wa Kidemokrasia uliotazamwa na wengi wa upande wa kushoto kama wa kusikitisha ambao haujaguswa na chama chao na taifa lao.
Kwa sababu hii, kampeni ya Mamdani ya kuwa meya imeangaziwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari,kuliko hata pengini uchaguzi wa Manispaa ya jiji hilo kubwa la Marekani.
Pia inamaanisha kwamba utendakazi wake kama Meya utafuatiliwa kwa karibu.
Miaka 12 iliyopita, Mwanasiasa wa chama cha Democratic Bill de Blasio alishinda kinyang’anyiro chake cha umeya wa jiji New Yor lililokuwa likikabiliwa na ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kijamii. Kama Mamdani, Wamarekani walio upande wa kushoto walikuwa na matumaini makubwa kwamba utawala wake ungetoa mfano wa kitaifa wa utawala huria wenye ufanisi.
De Blasio, hata hivyo, aliondoka madarakani miaka minane baadaye bila umaarufu mkubwa na akiwa na rekodi mchanganyiko ya mafanikio alipokuwa akipambana na ukomo wa mamlaka yake ya umeya kutekeleza sera mpya.
Mamdani atalazimika kukabiliana na mipaka hiyo hiyo – na matarajio yayo hayo.
Chanzo cha picha, Getty Images
Gavana wa New York Kathy Hochul, mwanachama mwenzake wa Democratic , tayari amesema anapinga sera yake yaudhibiti wa bei ya kodi za nyumba katika jiji hilo ambalo linajulikana duniani kwa kuwa na gharama kubwa ya kupangisha nyumba.
Na hata kwa ufadhili wa kutosha, Mamdani hataweza kutekeleza programu kwa upande mmoja.
Alifanya kampeni kama mkosoaji mkali wa wwamiliki wa makampuni na wafanyabiashara ambao wanaitaja New York City nyumbani kwao, na wameifanya Manhattan kuwa mji mkuu wa kifedha duniani. Ili kutawala vyema, pengine atalazimika kutafuta njia ya kufanya kazi nao kwa maslahi mapana ya jiji hilo, hata hivyo – mchakato ambao tayari ameanza katika wiki za hivi karibuni.
Pia amelaani mienendo ya Israel wakati wa vita vya Gaza na kuahidi kumkamata Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kama mhalifu wa kivita iwapo atakanyaga katika jiji la New York, ahadi ambayo inaweza kujaribiwa wakati fulani katika kipindi chake.
Hizi zote ni changamoto za siku zijazo hata hivyo. Kwa sasa, Mamdani atahitaji kuanza kazi ya kujieleza hadharani – kabla ya wapinzani wake kufanya hivyo.
Ingawa kampeni yake imepokelewa vyema kitaifa, bado ana kibarua cha ziada kuishawisho Marekani nzima
Kura ya maoni ya hivi majuzi ya CBS ilionyesha kuwa 46% Wamarekani walikuwa wakifuatilia uchaguzi wa meya wa New York. Hii inatoa fursa na changamoto kwa Mamdani na Wamarekani wanaoegemea mrengo wa kushoto.
Wahafidhina kutoka kwa Rais Donald Trump chini watakuwa wakijaribu kkumpinga meya huyo mpya kama tishio la kisoshalisti, ambaye sera na vipaumbele vyake vitaleta uharibifu katika jiji hilo kubwa la Marekani na kuelezea hatari ya kumpatia dhamana ya kuongoza taifa kwa ujumla.
Watakuza kila mashaka na kuangazia kila kiashirio hasi cha kiuchumi au takwimu za uhalifu.