Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid imeamua kumuuza mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 25, mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao kufuatia mwenendo wake alipotolewa uwanjani wakati wa mechi yao na Barcelona. (Bild – kwa Kijerumani)
Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo anataka kuondoka Real Madrid mwezi Januari, huku Arsenal na Tottenham zikimuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fichajes – kwa Kihispania)
Manchester United iko tayari kumwachia winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, ambaye anachezea klabu ya Aston Villa kwa mkopo, kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Sportsport)
Klabu ya Roma inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee mwezi Januari. (Calcio Mercato – kwa Kiitaliano)
Beki wa Inter Milan na Ujerumani Yann Bisseck, 24, anatamani kuhamia Uingereza, huku West Ham na Tottenham zikitarajiwa kuwa makao yake mapya. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)
Crystal Palace, Inter Milan na Juventus watachuana kuwania saini ya beki wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 30 Januari. (Caught offside)