MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa mkoa huo kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na kudhibiti majanga ya moto katika mkoa huo. Senyamule alitoa kauli hiyo jijini hapa wakati akizindua mitambo ya zimamoto na uokoaji.
“Nitoe rai kwenu kuhakikisha kila mmoja anachukua hatua za kukijinga na kudhibiti majanga ya moto,” alisema. Senyamule alisema mitambo hiyo itasaidia kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwani kwa kipindi cha mwaka 2025 kuanzia Januari hadi Oktoba kumekuwa na matukio 252 kati yake matukio ya moto ni 176 na maokozi ni 76 sawa na wastani wa asilimia 68.
Hivyo kuja kwa mitambo hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi na kukabiliana na matukio hayo bila kuleta madhara kwa binadamu. “Mitambo na magari haya yatatuwezesha kukabiliana na dharura kwa haraka na ufanisi zaidi, hivyo kuokoa maisha na mali za watu,” alisema.
Pia, mitambo itasaidia kuimarisha usalama kwa urahisi kwani mitambo hiyo ni ya kisasa. Upatikanaji wa mitambo hiyo utapanua wigo wa utoaji huduma kwa wananchi ukilinganisha na ilivyokuwa kipindi cha nyuma. SOMA: Dk Mpango atoa maelekezo miundombinu maji, zimamoto
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alisema mkoa una kila sababu ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mikubwa ambayo imewezesha kuletwa kwa mitambo ya kisasa, vituo vya polisi, vifaa na nyumba za askari. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Rehema Mende alisema serikali imetoa mitambo minane itawawezesha kufanya kazi kwa weledi
