
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Yannick Ndoinyo ameahidi kutekeleza ahadi zote alizoahidi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza leo nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kuapishwa amesema atakuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali kutekelezaji miradi ya serikali.

Amesema ikiwezekana bajeti ya miradi iongezeke hadi Sh bilioni 200 na hiyo ni kutokana na jiografia ya Ngorongoro kwa ujumla.

Aidha, amewataka wananch kuwa na imani na Bunge la Tanazania kwani ana uhakika watatekeleza Ilani ya CCM katika kila jimbo kwa maendeleo ya wananchi bila kubagua.