
RAIS Samia Suluhu Hassan atamuapisha Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 14.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka imesema hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu Mteule itafanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Dk Nchemba ameteuliwa na Rais Samia kuwa Waziri Mkuu na jina lake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 13, 2025.