DODOMA; Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amefungua Mafunzo kwa Wabunge leo Novemba 17, 2025 jijini Dodoma.

Mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwajengea uwezo wabunge kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo uendeshaji wa shughuli za Bunge, umuhimu wa Kamati za Bunge katika kufanikisha shughuli za Bunge na maadili ya viongozi.

Masuala mengine ni kuhusu haki na wajibu wa wabunge, diplomasia na itifaki za kibunge pamoja na uhusiano wa kazi baina ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *