JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza taarifa ya uongo kuhusu kutekwa kwa mwanamke aitwaye Hadija Jimmy, mwenye umri wa miaka 39.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao, ametaja watuhumiwa wengine ni Ashura Swalehe (48) na Vitus Joseph (34), ambao wote wanadaiwa kushirikiana kutengeneza simulizi la utekaji kwa lengo la kujipatia fedha.

Amesema watuhumiwa hao walidai kuwa Hadija alitekwa katika Kijiji cha Vumilia, wilayani Urambo mkoani Tabora na kutaka fedha kutoka kwa mume wa Hadija na walifanikiwa kupokea zaidi ya Sh milioni 1. SOMA: Polisi Songwe kuimarisha ulinzi uchaguzi mkuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *