Dar es Salaam: Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP-CENTRE) kimepokea ujumbe kutoka Wakala wa Usimamizi wa Mikataba ya PPP nchini Burundi (ARCP) kwa ziara ya mafunzo.

Ziara hiyo ya siku tano iliyoanza Jumatatu, imelenga kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika usimamizi wa miradi ya ubia.

SOMA: PPP nguzo ya utekelezaji Dira 2050

Hatua hii imeelezwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuijengea taasisi uwezo na kuimarisha mifumo ya PPP katika Afrika Mashariki.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-CENTRE, David Kafulila, alisema mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza uelewa wa usimamizi wa miradi na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu yenye manufaa kwa Tanzania na Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *