
ZANZIBAR; WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano Kombe la Shirikisho Afrika, timu ya Azam FC, imekubali kipigo cha bao 0-1 kwa Wydad AC ya Morocco kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mjini Zazibar usiku huu.

Huo ni mchezo wa pili kwa Azam kupoteza katika michuano hiyo, ambapo mara ya kwanza ilikuwa wikiendi iliyopita ilipokubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Maniema Union ya Jamhuri ta Kidemokrasia ya Congo (DRC).