
Rais wa Urusi, Vladmir Putin, sasa anasema atasitisha vita ya Ukraine ikiwa utawala wa Kiev utawaondoa wanajeshi wake toka kwenye miji yote inayodaiwa na Moscow, akionya kuwa tofauti na hapo atatumia nguvu kuichukua.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kauli hii anaitoa huku wanajeshi wake wakiendelea kuchukua maeneo zaidi ya mashariki mwa Ukraine, wakati huu Washington ikiongeza juhudi za upatanishi kujaribu kumaliza vita inayokaribia miaka minne.
Akizungumzia mapendekezo ya Marekani ambayo yamekosolewa na viongozi wa Ulaya, rais Putin amesema yanaweza kuwa msingi wa makubaliano ya siku za usoni, hata hivyo akisisitiza Jumuiya ya kimataifa kutambua maeneo iliyoyachukua toka kwa Ukraine, takwa linalopingwa vikali na Kiev.
Haya yanajiri wakati huu mpatanishi wa Marekani kwenye mzozo huo; Steve Witkoff, akitarajiwa kuzuru Moscow wiki ijayo huku katibu mkuu wa wizara ya vita ya Marekani akitarajiwa kutembelea Kiev.