
Wanasiasa karibu 40 wa upinzani nchini Tunisia wamehukumiwa kifungo cha miaka hadi 45 jela kwa kosa la kuhujumu usalama wa nchi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mahakama ya rufaa ya Tunisia imetoa hukumu hiyo kwa watuhumiwa hao, wengi wao wakiwa ni wakosoaji wa serikali ya Rais Kais Saied, ambao mwezi Aprili walikuwa wamepewa hukumu ya awali ya kifungo cha miaka 66, kwa kosa la njama dhidi ya usalama wa nchi na kosa la kuwa wafuasi wa makundi ya waasi.
Wengi wa watuhumiwa hao walikamatwa Aprili mwaka 2023 wakati wa maandamano ya upinzani dhidi ya serikali ya rais Kais ambapo walitajwa kama magaidi.
Miongoni mwa waliohukumiwa ni Ben Mbarek, Issam chebbi, Ghazi Chaouachi na Kamel Ltaief huku washtakiwa watatu wakiachiwa huru.
Mwanawe Chaouachi amesema kuwa walitarajia jambo hilo la kunyamazisha sauti za wapinzani hao kutoka kwa viongozi hao wanaopanga njama.
Umoja wa mataifa na wanaharakati wa haki za binadaam wameukosoa hukumu huo ila Rais Kais kwa upande wake ameishutumu jamii ya kimataifa kwa kuwatetea watuhumiwa hao akisema ni kuingilia maswala ya ndani ya nchi yake.