
Jeshi lililochukua madaraka nchini Guinea-Bissau limetangaza siku ya Ijumaa, Novemba 28, uteuzi wa Waziri Mkuu mpya, Ilidio Vieira Té. Kuhusu rais aliyeondolewa madarakani, Umaro Sissoco Embalo, ilijulikana Alhamisi kwamba aliwasili Dakar. Fernando Dias, ambaye alikuwa mshindanni wake mkuu katika uchaguzi wa urais, anamtuhumu kwa kupanga mapinduzi ili kuficha kushindwa kwake katika uchaguzi huo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku mbili baada ya jesi kumpindua rais Umaro Sissoco Embalo nchini Guinea-Bissau, jeshi limetangaza, kupitia taarifa kutoka kwa Rais wa Mpito, Jenerali Horta N’Tam, iliyotolewa saa sita mchana, uteuzi wa mkuu wa serikali siku ya Ijumaa, Novemba 28. Huyu ni Ilidio Vieira Té, ambaye hadi wakati huo alikuwa akishikilia wadhifa wa Waziri wa Fedha. Jeshi limefafanua kwamba pia Ilidio Vieira Té ataendelea kushikilia wadhifa wa waziri wa Fedha, hivyo kushikilia nyadhifa zote mbili.
Sherehe ya kuapishwa kwa Ilidio Vieira Té ilifanyika katika ukumbi mkuu wa ikulu ya rais huko Bissau, ambapo picha za viongozi wa zamani wa nchi hiyo, akiwemo Umaro Sissoco Embalo, zilikuwa zimewekwa kwenye kuta. Rais wa Mpito, Jenerali Horta N’Tam, Mkuu mpya wa Jeshi, Tomas Djassi, na takriban wanachama kumi wa Kamandi Kuu ya Jeshi walihudhuria sherehe hiyo ya kuapoishwa kwa waziri mkuu mpya. Jenerali Horta N’Tam alimtaja mkuu wa serikali kama “mfanyakazi mwenye bidii” ambaye ametaka kuendelea kufanya kazi naye “katika utawala mpya.”
Waziri Mkuu, ambaye aliapishwa baada ya kupiga picha rasmi ambapo wanajeshi walionekana wakiwa wamesimama imara, hakutoa taarifa yoyote: Ilidio Vieira Té alibaki nyuma kidogo wakati jeshi likitangaza uteuzi wake kwene nafasi ya waziri mkuu.
Ilidio Té Vieira alikuwa waziri wa fedha wa rais aliyeondolewa Umaro Sissoco Embalo, ambaye alikuwa mshirika wake wa karibu. Anashikilia. Ingawa mkuu mpya wa serikali anaelezewa kama mtu muhimu katika uhusiano kati ya Guinea-Bissau na washirika wake wa kiuchumi na kifedha, uteuzi wa Ilidio Vieira Té unatafsiriwa kama ishara ya utawala wa kijeshi unaokusudia kuihakikishia jamii ya kimataifa, lakini pia kama njia ya kuimarisha uhalali wake, siku chache tu kabla ya ziara iliyotangazwa ya ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS huko Bissau.
Watu wa Guinea-Bissau waliweza kuruhusiwa kutembea tena Ijumaa asubuhi na walipewa idhini na jeshi kufungua tena biashara zao.