Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuacha kumtafuta Askofu Josephat Gwajima kama walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake.
Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake.
“Mwacheni ajitokekeze tujenge umoja wa kitaifa, tushikamane kurudisha umoja wa kitaifa. Tumekutana na TEC, viongozi wa dini, wa mila na viongozi mbalimbali; twendeni sote kwenye jambo hili, tujitokeze tuhamasishe Tanzania yenye amani, huu ndio wito wa kiongozi wetu wa nchi.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumapili, Novemba 30, 2025 wakati akizungumza na wakazi wa Arumeru katika uwanja wa Magufuli Leganga, mkoani Arusha.
Waziri Mkuu amewataka Watanzania wakatae kushawishiwa na wanaharakati wanaochochea vurugu kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi. “Nimekuja kuwapa pole wananchi wenzangu, kwa niaba ya Samia.
Kabla ya mkutano huo, Waziri Mkuu alikagua uharibifu uliofanywa wakati wa vurugu za Oktoba 29, mwaka huu kwenye kituo cha polisi cha Kikatiti, Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, kituo cha mafuta Total Energies kilichopo Maji ya Chai ambavyo vyote vilichomwa moto na kuiba mali.
Waziri Mkuu ameonya dhidi ya mchezo unaotumika kuanzisha chokochoko ili kusambaratisha nchi pindi inapobainika kuwa na rasilimali. “Wanaanzisha chokochoko akituhumu baadhi ya nchi baeani Afrika kuhudika.
“Watanzania tuamke, tuchukue tahadhari. Kuna kamchezo kanachezwa. Wanajua Tanzania ina gesi asilia nyingi na inakaribia kuanza. Wanajua ikianza miradi hii, Tanzania itakuwa ya kwanza katika Afrika Mashariki na wala hatutahitaji kutoa mikopo ya wanafunzi.”
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)