‘Watanzania msikubali kutia doa taifa’‘Watanzania msikubali kutia doa taifa’

SHEHE wa Mkoa wa Mtwara, Jamaldin Chamwi amewasihi viongozi, wanasiasa, wananchi na wadau wote kutoruhusu dosari zozote zinazoweza kutia doa taifa la Tanzania.

Ameyaeleza hayo alipozungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani humo katika ofisi ya Jumuiya ya Waislamu (BAKWATA) iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo kuhusu kuwaomba Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Amesema ni vema kufuata mifumo iliyowekwa ili kuepuka uvunjifu wa amani kwani kwa miaka yote nchi ya Tanzania imejipambanua kwa kuishi na amani hali inayopelekea wageni kuvutiwa na taifa hilo. “Wakazi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla ni vema kujiepusha na kiashiria chochote cha uvunjifu wa amani kwa nchi kwani ikikosekana amani mambo mengi hayawezi kwenda,” alisema.

“Kama kawaida pasipo amani mambo mengi hayataenda kama vile inavyotakiwa kama vile ibada hazitafanyika kama kawaida lakini pia shughuli za kimaendeleo nazo hazitafanyika kama kawaida kwa hiyo suala la amani linapaswa kuzingatiwa wakati wote,” alisisitiza Chamwi.

Aidha, ametoa rai kwa viongozi na wananchi wote kuendelea kuheshimu mifumo, sheria, misingi iliyowekwa katika nchi na kuwasihi kushindana, kushauriana na kupingana kwa hoja bila kuvuruga amani ya nchi. SOMA: …Aagiza Polisi wasimtafute Askofu Gwajima

Sambamba na hilo, ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa rais na kwa hotuba yake iliyotoa kuhusu muongozo wa serikali yake namna ambavyo itafanya kazi katika awamu hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *