Rais Volodymyr Zelensky ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa X na kuongeza kuwa kumekuwa pia na visa vya uchokozi wa Urusi dhidi ya washirika wa Ukraine.

Zelensky ameendelea kuwatolea wito washirika wake kusaidia nchi yake katika kuimarisha ulinzi wa angani ili kuzuia mashambulizi ya Urusi.

Huku mzozo wa Urusi na Ukraine ukiendelea, vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi makali mapema Septemba 16 kusini mashariki mwa mji wa Zaporizhzhia nchini Ukraine.

Gavana wa jimbo hilo Ivan Fedorov amethibitisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 13, wakiwemo watoto wawili kutokana na mashambulizi hayo.

Fedorov amesema ripoti za awali zimesema magorofa 10 na majengo 12 binafsi yaliharibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *